Mary ainanga cheche BSS!
Mshiriki wa shindano la Bongo Star Search (BSS) mwaka 2009/2010 Mary Lucas ambaye hivi sasa anaimbia bendi ya Mjomba, ameamua kutema cheche kwa waandaaji wa mashindano ya BSS, Benchmark Production.

Mwanamuziki huyo chipukizi amesema kuwa, anaishukuru Bongo Star Search kwa kuweza kuinua vipaji vya wasanii wachanga na kuwafanya wasikike katika anga ya muziki, lakini suala la kuwaacha bila uelekeo linapoteza malengo ya shindano hilo.
"Kwa kweli nawashukuru sana ila kitu wanachokosea ni kuwainua wasanii wachanga halafu wakishamaliza wanawaacha pasipo msaada wowote na hivyo kujikuta wakishindwa kujiendeleza zaidi kimuziki" anasema.
Mary aliongeza kuwa pamoja na Bongo Star Search kuwasaidia wasanii, lakini bado uamuzi wake hauridhishi kutokana na kulalamikiwa na mashabiki kutotendeka haki katika kuwachagua washindi wa mashindano hayo.
Aliongeza kuwa yeye aliamua kuchukua uamuzi wa kujiunga na bendi hiyo ya Mjomba kutokana na kuvutiwa na muziki wake wanaopiga wa mirindimo ya asili ikiwa ni pamoja na kuendeleza kipaji chake.
Hivi sasa Mary anashiriki kuimba katika nyimbo zote za bendi hiyo alizozitaja kuwa ni pamoja na "Sheri mwilano" wimbo ambao unamzungumzia msichana ambaye amemkataa mume wake.
Kibao kingine alichoshiriki kuimba ni kile cha "Mama Siwema", "Nuru", "Upo nae", "Umoja wetu na Mzalendo". Bendi ya Mpoto inafanya maonyesho yake katika mahoteli na matamasha mbali mbali ya kitaifa
No comments:
Post a Comment