ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 7, 2010

Msisimko wa ndoa ya wana michezo


Shoaib Malik
                                                           Sania Mirza
                                                             
Nyota ya mchezo wa Kriketi nchini Pakistani Shoaib Malik amemtalaka mke wake wa kwanza akijiandalia ndoa yake na nyota ya mchezo wa tennis wa India Sania Mirza. Malik alidai hapo awali kuwa ndoa yake na Bi.Ayesha Siddiqui, ambaye ni Muislamu kutoka India haukusihi kwa sababu alidanganywa kuwa anafunga ndoa na mtu mwingine.
Kufuatia madai hayo Shoab Malik alihojiwa na polisi na pasi yake kukamatwa ili kumzuia asiondoke nchini India.
Mipango ya ndoa hii ya nyota wakubwa wa michezo barani Asia pamoja na kwamba Shoab alikanusha kuwa ana mke imezua hisia tofauti nchini India na Pakistan.
Kufuatia majadiliano ya usiku wa manane uliofanywa na wazee mcheza kriketi huyo amekiri sasa kuwa alikuwa na mke ambaye ni Ayesha Siddiqui na kwamba wameachana. Awali Malik alidai kuwa walikutana kupitia mtandao na kutimiza ndoa kwa simu jambo halali chini ya sheria ya kiislam. Lakini 
alisema baadaye kwamba picha alizoletewa na mtu aliyekutana naye walikuwa tofauti na kwa hiyo ndoa haikusihi.
Kufuatia mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na Bi.Siddiqui, Malik alihijiwa na polisi na kutakikana asiondoke nchini India. Madai hayo sasa yameondolewa na shughuli kubwa inatarajiwa kama ilivyopangwa.

No comments: