
Chama cha SPLM kimetangaza kususia uchaguzi katika majimbo kumi kati ya majimbo 15 yaliyoko kaskazini mwa nchi.
Hata hivyo chama hicho kitaendelea kushiriki uchaguzi katika eneo la kusini ambako kina umaarufu mkubwa.
Wiki jana chama cha SPLM kilitangaza kujiondoa kwenye mchuano wa urais, hatua iliyochukuliwa pia na vyama vingine vya upinzani.
Katibu Mkuu wa SPLM, Pagan Amum, amesema wanasusia uchaguzi kuonyesha kutoridhika kwao na hali ya usalama huko Darfur na hofu ya kuwepo na wizi wa kura.
Huu ndiyo uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi tangu mwaka wa 1986.
No comments:
Post a Comment