MVUA YAMWAGA KAMBARE MITAANI
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha mifereji yenye samaki kumwaga maji uswahilini na samaki aina mbalimbali wakiwemo kambare kutawanyika mitaani kama mwanahabari wetu alivyoshuhudia maeneo ya Mikocheni jijini Dar.






Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni, Adam Samweli, akivua samaki nje ya nyumba yao maeneo ya mikocheni.

Akiwa na kambare wake baada ya kumvua tayari kwa ajili ya kitoweo.

Huyu alimuhifadhi hapa, wakati akitafuta kitoweo kingine.

Kutokana na eneo hili lililopo karibu na Hospitali ya TMJ Mikocheni , kutopitika kirahisi, kijana huyu amepata ajira ya kuwabeba wasiotaka kukanyaga maji machafu kwa ujira wa shilingi 200.

Ofisi hii iliyopo Pembezoni mwa Hospitali ya TMJ inayoshughulika na mambo ya uchapishaji maarufu kwa jina la Luhango Stationary, ilibidi isitishe shughuli zake kutokana na kujaa maji.
No comments:
Post a Comment