ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 26, 2010

Ally Choki na harakati za utambulisho wa EXTRA BONGO



Wanamuziki wa bendi ya Extra Bongo leo wametia timu ofisi za Global Publishers kuelezea juu ya utambulisho wa bendi yao utakaofanyika Msasani Club ijumaa hii na kusema kuwa timu yake iko kamili.
Pichani, Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Prezidaa Ally Choki (wa pili kushoto) akiwatambulisha kwa wafanyakazi baadhi ya wanamuziki wake ambao alifika nao katika ofisi za Global. Aliyesimama kushoto akimsikiliza kwa makini ni Mhariri mtendaji wa magazeti hayo,Richard Manyota


Baadhi ya wanamuziki wa Extra Bongo wakiwa katika picha ya pamoja wakimsikiliza kwa makini Mhariri Mtendaji Richard Manyota (hayupo pichani) ambaye aliwaasa kufanya burudani safi siku hiyo
ya utambulisho wa bendi yao.


Choki (Kushoto) akisalimiana na kiongozi mwandamizi wa gazeti la Uwazi, Mzee Stambuli

No comments: