Timu ya Bongo DC
Timu ya Bongo Real FC
Timu ya MT.ZION FC
Kocha na mchezaji wa kutumainiwa wa BONGO REAL FC(jina tunalo) alinaswa na VIJIMAMBO akisema kwamba yeye na wenzake ambao ni wachezaji wa kutumainia,wamesikitika sana kwa wao kuwekwa benchi na wengine kutopewa Jezi,kwenye mechi iliyofanyika Jumapili June 20 uwanja wa Kalmia ambapo timu ya Bongo DC ilibanjuliwa 3-1 na timu ya MT.ZION inayomilikiwa na George Mwasalwiba.Kitendo hicho kimepelekea kwa yeye binafsi na wachezaji wenzake wenye uchungu na jina la Bongo,kuanzisha timu inayoitwa Bongo Real FC na kuomba mechi na timu ya MT.ZION.
Tarehe bado haijapangwa,kwa sasa tupo kwenye mazoezi makali,chini yangu,alisema kocha mchezaji huyo,mechi kama ile ya juzi sio mechi ya kufungwa,kufungwa walijitakia wenyewe.
Alipoulizwa je wachezaji hao ni wakina nani,aslisema kwa sasa ni mapema mno kuwataja,pili si jambo zuri unapokuwa vitani kumpa mpinzani wako mbinu ya timu aina gani ulionayo,sisi tutakapokua tayari tutaomba mechi na MT.ZION na tutawaonyesha kile Bongo DC ilichoshindwa kukifanya.
No comments:
Post a Comment