ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 12, 2010

DSTV wazindua rasmi kombe la Dunia


Na Andrew Chale
KAMPUNI  ya Multchoice  Tanzania inayosambaza vifaa vya DSTv nchini jana usiku ilizindua rasmi michuano ya kombe la Dunia katika halfa maalum iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa michezo nchini.
Katika sherehe halfa hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Savannah uliyopo ndani ya Hoteli ya Paradise Suite City Centre, jijini Dar es Salaam, wadau hao walijumuika kwa pamoja na kufurahi shangwe hizo zilizo kuwa zikirushwa moja kwa moja kwa kutumia screen za kisasa zilizo kuwa zikitumia HD.
Ufunguzi huo ambao DSTv  kupitia channeli zake za Super Sport ambazo zinaonyesha michuano hiyo yote 64, ndiyo iliyo na mamlaka ya kurrusha matangazo ya kombe hilo .
Kwa upande wake Afisa Habari wa Multchoich nchini, Barbra Kambogi alisema kuwa wateja waendelee kujitokeza kununua vifaa hivyo vya kisasa kwa bei nafuu na kupata kushuhudia michuano hiyo iliyo na mvuto duniani kote.
“Tunawaomba wateja kujitokeza kununua vifaa vya DSTV na kubahatika kupata kushuhudia vipindi mbalimbali pamoja na michuano hiyo’ alisema Barbra.
Wadau waliojitokeza katika halfa hiyo walipata kuburudika pamoja na kupuliza vuvuzela ambayo ni maalufu nchini Afrika kusini pamoja na kubadilishana mawazo..

No comments: