Na Andrew Chale
MAITI ya mtoto mchanga jinsia ya kike inayodhaniwa kuwa na umri wa siku moja imeokotwa barabarani huko maeneo ya Charambe, ikiwa imetupwa na mtu asiye julikana.
Akiongea na waandishi wa Habari ........jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime alisema kuwa tukio hilo lilitokea ,,,,,,,,,leo,,,,,,,,juzi majira ya saa 12 jioni ambapo maiti ya kichanga hicho kiliokotwa na wapiti njia.
Kamanda Msime alisema kuwa uchunguzi wa kumsaka mtu aliyekitupa kichanga hicho unaendelea na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile alisema kuwa katika msako wa dolia wa jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ya Ilala, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 kwa makosa ya kukutwa na dawa za kulvya.
Kamanda Shilogile alisema kuwa jeshi ilo liliendesha msako huko maeneo ya Tabata na kufanikiwa kuwakama watuhumiwa watano wakiwa na kete saba za dawa zizaniwazo kuwa ni za kulevya.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ramadhan Kisesa(26), Salum Jumbe(23), Juma Ayubu(23) na wenngine saba waliokaamatwa katika msako huo wakiwa na bangi kete tano ni pamoja na Amina Said(26)Jamal Hamad(29), Ally Juma(29) na wenzao .
Watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na jeshi hilo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani kesho.
No comments:
Post a Comment