ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 27, 2010

Kipute cha Bongo DC na MT.ZION nguvu sawa

Timu ya Bongo DC
Timu ya MT.ZION
kidumbwe cha MT.ZION na BONGO DC
Mmiliki wa MT.ZION,George Mwasalwiba
mchezaji wa kiungo Shaka alikua mwiba na msumari wa MT.ZION
Timu ya MT.ZION kila siku inapocheza na BONGO DC hua inapata ushindi wa ubwete lakini leo walikua wanaomba mpira uishe angalau wapate suluhu kuliko kuadhiliwa na Bongo DC.

Mpambano wa leo haukupata washabiki wengi kutokana na mvua iliyonesha muda mchache kabla ya mpambano.

Mechi ilianza taratibu kwa kila timu kusoma mchezo wa mwenzake huku Mt,Zion  ikionekana kulinyemelea goli la Bongo DC.Kunako dakika ya 28 ya mchezo kiungo wa Bongo DC Shaka alipiga kombora lililomuacha kipa mahili wa Mt.Zion,Willy akigagaa huku nyavu zikitikisika na refa Kenyata akisema ni goli safi weka kati.

Mpaka mapumziko Bongo DC walikua mbele kwa goli moja,katika jambo lililokua si la kawaida,mmiliki wa Mt.Zion alimkataa mshika kibendera,Susa ambaye  kawaida huchezea Bongo DC,kwa madai anaifundisha timu yake jinsi ya kucheza.

Kitu kingine ambacho kilikua si o kawaida ni kocha wa Mt.Zion Sir Benja alikua kimya kuliko kawaida ya kocha huyu hua mwenye makeke mengi awapo uwanjani na hii ni kutokana na timu yake kua nyuma goli moja muda mrefu
kipindi cha pili kilianza kwa Mt.Zion kuendelea kulisakama goli la Bongo DC na huku Bongo DC wakijaribu kupata goli la pili.

Kunako dakika ya 65 kipindi cha pili Mt.Zion walijipatia bao la kusawazisha,lililowazindua usingizini wapinzani wao,baada ya bao hilo walianza kuliandama goli la Mt.Zion kama nyati aliyejeruhiwa.

kunako dakika ya 76 shaka aliachia msumari mwingine nje ya kumi na nane uliomucha golikipa wa Mt.Zion akigala gala asijue la kufanya lakini kabla goli halijaingia refa alishapuriza kipenga Shaka alifanyiwa mazambi kabla ya kuupiga mpira huo,rafu iliyomtoa nje asiweze kuendelea na mchezo kutokana na kuumia vibaya.badala yake aliingia Saad na kusababisha penati kunako dakika ya 85 kwa kuchezewa ndani ya kumi na nane.

Mchezaji wa kioungo Gilles alikosa penati hiyo kwa kumpigia kipa mkononi.mpaka 90 MT,ZION 1-1 Bongo DC

No comments: