Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Mr. II au Sugu kama anavyojulikana na wengi, ameeleza sababu za kukamatwa kwake leo na jeshi la Polisi nchini. Akielezea sakata hilo, Mr II amesema kuwa alikatwa kuhusiana na mstari mmoja uliyomo kwenye wimbo wake ambao unapatikana kwenye albamu ya Anti Virus ambayo hivi sasa inasambazwa bure mtaani kwa mashabiki wa muziki huo. Katika wimbo huo, Mr. II amedaiwa kutishia kuua pale anaposema I wanna kill you, jambo ambalo amesema limemshangaza kwa sababu maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Mr II, ambaye amedai kukamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, ametakiwa kuripoti tena kesho kutwa kituoni hapo.
Mr. II, pamoja na wasanii wengine wa Hip Hop nchini, wamerekodi nyimbo kadhaa za hip Hop na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Bongo. Awali, msanii mwingine wa Hip Hop, Dudubaya, naye alirekodi albamu yenye nyimbo kama hizo na kuiita NGURUWE.
Tukio la kukamtwa kwa Mr. II, limekuja siku tatu tu baada ya kutangaza kujiunga na chama cha siasa(CHADEMA) Ijumaa iliyopita na leo alitarajiwa kutangaza nia ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho mkoani Mbeya.

PICHA NA RICHARD BUKOS NA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLSHERS
No comments:
Post a Comment