
MASHABIKI wa soka katika maeneo mbalimbali wameonyesha kukerwa na mwenendo wa timu za Afrika zinazoshiri michuano ya Kombe la Dunia kwa kuamua kuacha kuzishangilia kwa madai, wanapoteza nguvu zao bure.
Mashabiki waliokuwa wakihojiwa na televisheni za Super Sport na SABC katika vipindi vilivyojumuisha waandishi mbalimbali wa habari waliojitokeza kuripoti michuano ya Kombe la Dunia wamesema hawaoni sababu ya kuendelea kuziunga mkono timu hizo.
Katika michuano ya Kombe la Dunia, Afrika inawakilishwa na wenyeji Afrika Kusini, Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria na Cameroon lakini zimeonekana kuwa na mwendo wa kusuasua wakati hatua za awali za makundi zinaenda ukingoni.
Hali hiyo imezua hofu kwa mashabiki wengi wa Afrika lakini wale wanaotoka katika jiji hili wameona hakuna haja ya kuendelea kuziunga mkono timu hizo kwa kuwa zinawaumiza roho.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameamua kuendelea kuziunga mkono hadi mwisho, huku wakiamini huenda kukawa na mabadiliko katika hatua za mwisho.
Tokea kuanzishwa kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1930, Afrika ambayo mwaka huu kwa mara ya kwanza michuano inafanyika kwenye udongo wake haijawahi haijawahi kuvusha timu zaidi ya hatua ya robo fainali.
Mwaka huu kwa mara ya kwanza, bara hili limeshirikisha timu nyingi zaidi, sita lakini inaonekana mwenendo wake unaweza ukazifanya zitolewe mapema na kushindwa kuvunja rekodi ya hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment