ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 20, 2010

Eti foleni za magari,Dalili ya maisha Bora!

kikwete.jpg
Wakati kumekuwa na mjadala juu ya kufanikiwa au kushindwa kwa kaulimbiu ya 'Maisha bora kwa kila Mbongo', iliyotumika kumnadi Rais JK wakati wa kampeni mwaka 2005, kiongozi huyo ametolea mfano foleni za magari ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuwa ni moja ya dalili za maisha bora.

JK alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza ktk sherehe iliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Dsm kwa ajili ya kumpongeza kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais.

"Hapa Dsm taabu ya msongamano wa magari inaonesha hali ya maisha ni bora, sasa tunahangaika jinsi ya kuondoa msongamano, kuanzia mwakani tutaanza kujenga barabara za juu," alisema Rais Kikwete.

1 comment:

Anonymous said...

HUU NI UPUMBAVU USIO NA KICHWA WALA MIGUU..I FEEL SORRY FOR MY COUNTRY..INIESTA