ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 14, 2010

FRED MPENDAZOE NA WENZAKE WAJIUNGA CHADEMA!

Mpendazoe akikabidhiwa kadi.
Muda mfupi uliopita, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amewapokea waliokuwa viongozi waandamizi wa CCJ, Richard Kiyabo aliyekuwa Mwenyekiti, Dickson Ng’hily aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCJ Bara na Fred Mpendazoe aliyekuwa Msemaji Mkuu wa CCJ Taifa.

Viongozi hawa wamejiunga rasmi na CHADEMA mchana huu na kukabidhiwa kadi na Mbowe mbele ya Waandishi wa Habari.

Pamoja na kujiunga na CHADEMA Viongozi hawa pia wametoa tamko rasmi la kwanini wamejiunga na chama hiki, Vile Vile Viongozi hawa wametangaza nia ya kugombea Ubunge kupitia CHADEMA kama ifuatavyo;

Dickson Ng’hily -Kugombea Jimbo la Temeke
Richard Kyabo-Kugombea Jimbo la Bukene
Fred Mpendazoe-Kugombea Jimbo la Segerea
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akihutubia mkutano huo. 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCJ (kulia) akikabidhiwa kadi na Freeman Mbowe. Katikati ni Mpendazoe.

Dickson Ng’hily (kushoto) akikabidhiwa kadi na Mbowe.

Mpendazoe akielezea sababu zilizomtoa CCJ na kumhamishia CHADEMA ambapo alisema alifanyiwa hila za kunyimwa usajili wa kudumu na kwamba alichofanya ni sawa na rubani kubadili gea akiwa angani.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: