ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 25, 2010

PWEZA PAUL APATA TUZO KUTOKA HISPANIA

"Paul" aliyejulikana kama "pweza mganga" akizawadiwa jezi na medali ya shaba mjini Oberhausen, Ujerumani.
PWEZA "Paul" aliyeweza kutabiri vyema matokeo ya mechi za soka za Kombe la Dunia mwaka huu zilizofanyika nchini Afrika Kusini, ametunukiwa zawadi ya jezi na medali ya shaba kutoka Hispania. 

Tuzo hiyo ilitolewa kwa kiumbe huyo kwenye jiji la Oberhausen magharibi mwa Ujerumani katika bwawa la kufugia viumbe wa majini la Sea Life Aquarium. Pia Paul amechaguliwa kuwa 'rafiki wa upendeleo' wa mji wa Carballino.
Pweza huyo alitabiri vyema mechi zote sita ambazo Ujerumani ilicheza katika mashindano hayo mwaka huu, ambapo alitabiri pia kwa usahihi ushindi wa Hispania dhidi ya Uholanzi, pamoja na ushindi wa Ujerumani kunyakua nafasi ya tatu dhidi ya Uruguay


CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: