ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 9, 2010

Kama amekuacha ya nini kumsujudia, mambo muhimu ya kuepuka ni haya

Wapenzi wengi baada ya kuachana huwa wanapata tabu sana hasa wakifikiria jinsi walivyokuwa wakiishi kwa mazoea. Wengi hukonda na kupoteza ‘appetite’ ya kila kitu ikiwa ni pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa wale walioko makazini.

Ni kweli enzi limevunjika na umeumia kwanini usizoee na kuona kuwa kuna wengine wengi waliokuwa wanatamani uachwe wapate wao? Hebu jiulize je huyu mwanaume/ mwanamke nilizaliwa naye? Je, kama angefariki ungeenda naye kaburini kwani? 

Ukishajiuliza maswali hayo cha kufuata ni hiki ambacho nataka nikufundishe wewe unayeona huwezi kuishi bila yeye kwani wengi hushindwa kuvumilia na kufanya haya akidhani huenda anaweza kumshawishi akarudi ...

1. Baby nakubembeleza 

Usijaribu kabisa kutumia lugha hii, siwezi kuishi bila wewe, naomba unisamehe turudiane. Maneno haya kumbuka kuwa ulikuwa ukimtamkia wakati bado anazo hisia kwako, mpaka mnafikia kuachana jua hana jipya tena na hata akitaka kurudi jua ni tamaa tu ya mwili wala si mapenzi kwako. Cha muhimu ni kumpotezea kabisa.

Mwenzio anakucheka unapokuwa unamtumia sms au unampigia simu, anakuona bwege kweli, mwanzo alikuwa anainjoi kubembelezwa lakini baada ya mapenzi kuisha anakuona kituko tu, usijaribu kutumia simu yako au computer yako kuwasiliana naye.

3. Mapenzi ya kuhisi

Watu wengi siku hizi hutembelea mitandao mbalimbali ikiwa ni pamoja na Face book akikuta tu mtu kaandika mada inayofanana na yeye anaanza kuwaambia wenzake unaona huyu bado ananijali, atakuwa ananipenda tu hataki kuonekana anarudi. Hata kama ukweli ni huo kwanini umuongelee yeye mara kwa mara? 

Yeye ni nani mpaka akuumize, haya tunayaita mapenzi ya hisia mwenzako si ajabu hata hakuwazii kabisa wewe unaumia kwa maneno yake machache, je kama anao wengi na si wewe ambaye anamuandikia? Huoni kama utakuwa unaumiza nafsi yako pasipo yeye kujua.

4. Kujipitisha pitisha
Unajua kabisa mpenzi wako mliyeachana anakaa Tabata na wewe unaanza mitoko ya huko ili mradi tu akuone, unatafuta mawasiliano na rafiki zake, ili tu utafute njia ya kuonana naye kwa sababu gani ufanye hivyo? Anakudharau tu hapo hakuna penzi tena cha kufanya wewe ni kuangalia mbele, kwa kufanya hivyo atakuheshimu daima.

Lakini kama utamfata fata atakachotaka yeye ni kukufanya chakula cha hamu na kisha anakupotezea, pale anapokuhitaji siku zote atakutafuta kisha atakuachia maumivu.

5.Kuunda urafiki na mpenzi uliyeachana naye

Mmeshaachana na kila mtu anajua sasa kama mmeachana unajifanya mnataka kuendeleza urafiki, huo ni ugonjwa tena mbaya sana, hakuna urafiki hapo ni kudanganyana tu. Hebu jiulize unaweza ukamuuliza huyo mliyeachana mpenzi wake anaendeleaje au familia yake? 

Je atakujibu? Je utakuwa uko sahihi kumuuliza swali hilo au utakuwa mnafiki? Hilo ni swali nawaachia wasomaji wangu nahisi mtanipa majibu kupitia mawasiliano niliyotoa hapo chini.
Kupitia majibu yenu mada yetu itaendelea wiki ijayo.

No comments: