ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 9, 2010

MAZISHI YA P. DIDDY KUGHARIMU MILION 5/=

Mtangazaji wa kituo cha runinga cha TBC, Maimartha Jesse, akifarijiwa na waombelezaji katika msiba huo. 
ALIYEKUWA Mkurugenzi Msaidizi wa Bendi ya Diamond Musica, (Vijana Classic), Perfect Kagisa, aliyefariki jana baada ya kuanguka ghafla eneo la Lumumba, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwili wake unatarajiwa kuzikwa kesho Makaburi ya Kinondoni jijini. 

Msemaji wa shughuli za mazishi hayo ambaye ni mtangazaji maarufu wa kituo cha runinga cha TBC, Benny Kinyaiya, amesema kwenye msiba huo ambao unafanyika nyumbani kwao marehemu Kinondoni-Mwanamboka, kwamba zinahitajika milioni 5/= ili kukamilisha bajeti ya mazishi hayo.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Bibi wa marehemu ambaye pia alikuwa mlezi wake, Imelda Rwebangira, akisaidiwa na waombolezaji wakati akiingia msibani.
Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Jacob Steven (aliyenyoosha mkono) maarufu kama JB, akitoa pole kwa wafiwa.
Mwendeshaji wa shughuli hiyo, Ben Kinyaiya, akiwatangazia ratiba ya mazishi waombolezaji.
Ben Kinyaiya akisisitiza jambo fulani kwa Mkurugenzi wa bendi ya Akudo Impact, Michael Andrew, wakati akiondoka kwenye msiba.
Maimatha Jesse (kulia) akinong’onezwa jambo la Husna Iddi aka Sajenti Kimwana Manywele.
Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani ni pamoja na wasanii wa filamu Jacqueline Pentzel aka Jack wa Chuz (kushoto), Snura Antony na Kimwana Manywele Halima Haroun (kulia).
Sehemu ya ndugu waliofika katika msiba huo wakiwa katika nyuso za masikitiko.
Jack wa Chuzi akiwa msibani.
Snura Anthony akiwa na masikitiko baada ya kumpoteza mpendwa wake.



PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

No comments: