ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 19, 2010

KANUMBA ASIKIA KILIO CHA MZEE KIPARA

Baada ya Mzee Kipara kulalamika kwenye gazeti la mastaa la Amani kuwa wasanii Kanumba na Ray wamemtupa ili hali yeye ndiye aliyewafundisha sanaa, hatimaye kilio chake kimesikika baada ya Kanumba kumtembelea nyumbani kwake Kigamboni mapema wiki hii. Katika ziara hiyo ya kushitukiza, Kanumba aliongea na Mzee Kipara kuhusu matatizo yake ya miguu ambayo imekuwa ikimsumbua kwa muda mrefu sasa ambapo msanii huyo, mwenye mafanikio katika sanaa ya filamu nchini, aliahidi kumtafutia daktari bingwa wa kulishughulikia tatizo lake. Wakati akiondoka, alimuachia pia na kiasi cha fedha cha kujikimu na kumuahidi kuendelea kuwasiliana naye mara kwa mara. Mashabibi wa Kanumba wamekipongeza kitendo cha kukumbuka alikotoka na kumkubuka mzee Kipara ambaye ana mchango mkubwa katika mafanikio yake. Wasanii wengine wameombwa kuiga mfano huo.
Kanumba akisalimiana na Mzee Kipara nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es salaam

Kanumba akimkabidha Mzee Kipara kiasi cha fedha za kujikimu
...baada ya maongezi yao, Mzee Kipara alimtoa Kanumba na kuagana naye

No comments: