\Pichani ni Mayor Mlima(mwenye suti)),Bruno Mazali(shati Dark blue)na mfanyakazi wa mortuary(t-shirt nyeupe)wakisaidia kutoa mwili wa marehemu Andrew Pesa Igala tayari kwa safari kuelekea Tanzania ambako mwili unatarajiwa kufika siku ya Alhamisi Sept 9 na BA
Mwili wa marehemu Andrew Pesa Igala Ukiingizwa kwenye gari
Bruno mazali akishauriana jambo na mfanyakazi wa Mortuary
Bruno Mazali akimuaga kwa mara ya mwisho na kuutakia mwili wa marehemu Andrew Igala safari njema
Eva Msowoya akiutakia mwili wa marehemu Andrew Igala safari njema Tanzania(Picha kwa hisani ya Mayor Mlima)
SHUKRANI
Familia ya Igala inapenda kutoa shukrani zake kwa Ubalozi wa Tanzania,Washington,DC,PG Hospital na Watanzania wote,Marekani hususani,Washington,DC,kwa moyo wa upendo mliouonyesha kwa ndugu yetu mpendwa,marehemu Andrew Pesa Igala,kwa ushirikiano na mshikamano wenu wa hali na mali,hatimae kuwezesha kusafirishwa kwa mwili wa marehemu Tanzania,hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na wema huu,bali tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie saba mara sabini.
Tulimpenda sana Andrew ila Bwana amempenda zaidi jina lake lihimidiwe
No comments:
Post a Comment