Ndugu wa Tanzania,
Siwezi kupata maneno mazito vya kutosha kutoa Shukrani zangu za dhati. Ukweli Jumapili Septemba 5,2010 ilikuwa siku ya kihistoria kwetu. Asanteni sana kwa kuja kushirikia Misa takatifu ya kihistoria Pale Capuchin College Washington DC. Tumeachiwa Changamoto la kudumisha utamaduni huo wa kumsifu na kumwadhimisha Mungu kwa Lugha Yetu ya Kiswahili. Pia hii itatusaidia kuwa karibu zaidi sisi kwa sisi na kuweza kujipatia mahitaji ya kiroho bila mahangaiko makubwa.
Tafadhali kama unayo mawazo ya kuborasha ututumie mara upatapo nafasi.
Padri Pisa Shukrani za Pekee kwa ukarimu wako kutupatia mahali pa kushibisha Roho na mwili. Tafadhali toa shukrani hizi pia kwa Jumuiya yako.
Kwaya Toka St. Camilus. Tuwashukuruje? Mungu tu anaweza kuwarudishia kwa ukarimu wenu. Wote walioandaa vyakula na Vinywaji






No comments:
Post a Comment