
Na Mwandishi wetu
LEO ndiyo mwisho wa ubishi, baada ya kukaa kambini kwa takribani mwezi mmoja na kufanya safari mbalimbali za utalii na kufikia kutaka kuzama katika Bahari ya Hindi, Mshindi wa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania anapatiakana katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Shindano hilo lenye msisimko mkubwa litamaliza ubishi wakati majaji watakapomchagua mshindi mmoja ambaye ataibuka na gari aina ya Hyundai i10 pamoja na shilingi Milioni 10.
Jumla ya warembo 30 watapanda jukwaani kuonyesha ‘ulimbwende’ wao bila ya kusahau vipaji na uwezo wao wa kujieleza kwa kujibu maswali ya majaji.
Mbali na zawadi, mshindi wa shindano hilo atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika shindano la warembo wa dunia, Miss World litakalofanyika Sanya, nchini China.
Habari kwa hisani ya Global Publishers
No comments:
Post a Comment