Maelfu ya wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wengine walianza kumiminika kwa wingi kwenye viwanja hivyo kuanzia saa sita mchana na hadi kufikia saa 9 alasiri hali ilikuwa imebadilika na eneo hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi.
Hilo la umati lilithibitishwa na Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Amani Abeid Karume, aliyesema kwa hali ilivyokuwa kwenye mkutano wa jana haijapata kutokea wananchi wengi kujitokeza kwa wingi.
"Nipo nyuma ya Dk. Shein, leo si siku yangu ya kampeni, lakini nimekuja hapa mahususi kusema namuunga mkono, nipo naye bega kwa bega na nitamuunga mkono kuhakikisha anashinda.
![]() |
| Umati wa wafuasi na wanachama wa CCM waliojitokeza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Ali Mohammed Shein, kwenye viwanja vya Kibandamaiti, mjini hapa jana. (Na Mpigapicha Wetu). |

No comments:
Post a Comment