ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 27, 2010

Ali Kiba atua Marekani,kupiga kolabo na R.Kelly

Wa Kwanza Kulia ni Msanii Machachari wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Ali kiba akiwa na wenzake wa ONE8 group wakiredi single yao pande za chi-town US.Wasanii hao ni pamoja na 2-Face ,Navio,Amani,4×4 na wengineo.


Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, msanii Ali Kiba ametua Chicago,IL,nchini Marekani kwa ajili ya kugonga ngoma ya pamoja na baadhi ya mastaa wa Afrika, kabla ya kufanya kolabo na staa wa kimataifa, Robert Kelly wa pande hizo.

Kwa mujibu wa msemaji wa ishu hiyo, Christine Mosha ‘Seven’, Ali Kiba ataungana na mastaa wengine kutoka Afrika wakiwemo Navio (Uganda), Amani (Kenya), 2Face (Nigeria), Fally Ipupa (Congo), JK (Zambia), 4x4 (Ghana) na wengine waliopata nafasi hiyo kupitia utafiti uliofanywa na Kituo cha Televisheni cha MTV Base wa kutafuta wasanii wakali kwa nchi za Afrika.


No comments: