Filimbi ya upigaji kura imeshapulizwa na tayari hivi sasa wananchi wapo vituoni na wengine tayari wameshapiga kura. Hali mpaka sasa hivi ni shwari katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam na hakuna foleni ndefu katika vituo vingi vilivyotembelewa na mtandao huu. Pichani ni baadhi ya wapiga kura wa kituo cha Amana Ilala.
UTARATIBU:
Ukifika kituoni, kitu cha kwanza ni kuangalia jina lako kama lipo kwenye orodha ya majina iliyobandikwa kituoni hapo, ambayo imepangwa Alphabetically. Na katika kituo kuna vyumba zaidi ya kimoja na watu wanaingia kulingana na majina yao. Ukiona jina lako, wasimamizai watakuelekeza chumba chako ambapo utapanga foleni na zamu yako ikiwadia utaingia chumbani ambako utamkuta mkaguzi wa kituo ambaye atasoma jina lilioandikwa kwenye kadi yako kwa sauti kubwa kwa jili ya mawakala wote wa vyama kusikia jina lako. Baada ya hapo, utaenda kwa msimamizi wa pili ambaye atakupatia karatasi tatu za kupigia kura, za Rais, Mbunge na Diwani. Utaenda sehemu malaumu ya kuandika ambapo utatiki unayemtaka, katika karatasi zote tatu, utazikunja na kudumbukiza katika masanduku matatu tofauti, kila moja likjitegemea. Mwisho unapita kwa msimamizi wa mwisho anakuwekea wino kwenye kidole chako cha mwisho na Off u Go...!!
...ubao wa majina ya wapiga kura unaoweza kukutana nao katika kituo chako kama kituo cha Amana Ilala
...hakuna misururu mirefu ya wapiga kura, hata hivyo hali inaweza kubadilika baadae hivyo wasimamizi wametakiwa kuwa wapesi ili kuwahi muda wa mwisho uliowekwa na Tume wa saa kumi jioni.
PICHA: Abdaalha Mrisho/GPL
No comments:
Post a Comment