ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 8, 2010

ABIRIA ABAMBWA NA NYOKA, NDEGE KWENYE NDEGE

Baadhi ya nyoka waliokuwa katika mizigo ya abiria huyo akitokea Arabuni.
ABIRIA mmoja katika ndege amekamatwa akiwa na mfuko uliojaa nyoka na ndege wakati akisafiri katika ndege iliyokuwa inakwenda Marekani kutoka Falme za Kiarabu.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Abu Dhabi walishangaa baada ya kumwomba abiria huyo akifungua begi lake na kuwakuta viumbe hao, hiyo ilifuatia ofisa mmoja kuona kitu kilichokuwa kinatembea katika sanduku moja la karatasi la abiria huyo kabla ya kupanda kwenye ndege.

Nyoka hao walikuja kugundulika kuwa ni chatu wasiokuwa na madhara. 

Hata hivyo, abiria huyo aliruhusiwa na polisi kuendelea na safari yake lakini bila wanyama hao.


                               CHANZO:GLOBAL PUBLISHER

No comments: