ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 16, 2010

Waziri ataka moshi wa Feri usingie Ikulu

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo.
Feri kuboreshwa
Mahija Mpera
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo, ameuagiza uongozi wa Soko la Samaki la Feri, jijini Dar es Salaam, kuboresha majiko yanayotumika katika kukaangia samaki, ili kuepusha moshi kuyafikia maeneo ya Ikulu.
Waziri huyo alitoa agizo hilo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa soko jilo na baadhi ya wafanyabiashara wa samaki katika soko hilo.

Alisema majiko mengi katika sokoni hilo ni ya muda mrefu na kwamba yameharibika kiasi cha kusababisha moshi, kufika Ikulu, jambo ambalo ni la aibu hasa kwa wageni wa mataifa mbalimbali wanaokwenda Ikulu.


Alisema pamoja na tatizo la moshi, soko hilo pia linakabiliwa na tatizo la uchafu wa vyoo na chemba za maji machafu.

Waziri Mathayo alisema kwa kuzingatia athari za hali hiyo, kuna hana kwa uongozi wa soko, kuchukua hatua za haraka za kuboresha mazingira ya soko.

Alisema uchafu katika maeneo ya soko, unahatarisha afya za wafanyabiashara na wateja kwa jumla.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara walimlalakia kitendo cha wenzao, kushirikiana na wafanyabiashara wa nje wanaofanya kazi ya kusafirisha samaki kwenda nje ya nchi.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Winfrida Mwambu, alisema kumekuwepo na wimbi la wafanyabiashara wa Kichina, wanaosafirisha samaki kwenda nje huku wakishirikiana na wafanyabiashara wenye leseni halali wa hapa nchini.


Akizungumza tatizo hilo, Mathayo alielezea kushangazwa kwake na kwamba wafanyabiashara hao, si wazalendo wa nchi yao.

Alisema yeye kama kiongozi mkuu katika wizara inayoshughulikia sekta ya uvuvi, kamwe hawezi kufumbia macho watu wanaojihusisha na biashara hiyo na kuwataka viongozi pamoja na wafanyabiashara hao kumpa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara hiyo ili wachukuliwe hatua.

                                        CHANZO:MWANANCHI

No comments: