
NAAM tumekutana tena katika safu yetu ya mahusiano na mapenzi katika mwaka 2011. Najua kila mtu atakuwa na aliyovuna mwaka uliopita wapo waliojuta na kuyachukia mapenzi. Lakini wapo walioyafurahia na kuuona mwaka kwake uliisha vizuri.
Katika safari ya maisha ambayo muhimili wake mkubwa ni mapenzi basi lazima uelewe hakuna njia ya tambalale mwanzo hadi mwisho. Muhimu ni kujiuliza mwaka uliopita ulijikwaa wapi sio kuangalia ulipoangukia.
Katika safari ya maisha ambayo muhimili wake mkubwa ni mapenzi basi lazima uelewe hakuna njia ya tambalale mwanzo hadi mwisho. Muhimu ni kujiuliza mwaka uliopita ulijikwaa wapi sio kuangalia ulipoangukia.
Napenda kuzungumza na wote ambao mwaka uliopita waliumizwa na mapenzi ya njia moja ama nyingine kufikia hatua ya kujikatia tamaa ya maisha. Lakini kwa wale ambao kwao mambo yalikwenda vizuri ni nafasi nyingine ya kuongeza upendo na kuondoa makosa madogo madogo ambayo huwa sawa na ufa ukizidi huangusha nyumba.
Ila kwa wenzangu ambao wameuona mwaka 2010 kuwa ni mwaka wa mikosi. Kutokana na kupokea simu na ujumbe mwingi katika kona hii na kuonyesha jinsi gani watu wanavyoumizwa na mapenzi.
Nachukua fursa hii kuwaeleza wote ambao wameumizwa na mapenzi na kufikia hatua ya kuiapia mioyo yao kuwa hawatapenda tena au hawatapendwa tena. Hapa napenda kuliweka wazi jambo hili kwa kuwaeleza kuwa.
Katika safari ya maisha kuna mambo mengi ya kufurahisha na kukatisha tamaa, lakini vyote vipo kwenye safari ya maisha kinachotakiwa ni wewe kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza mbele yako.
Napenda kukueleza mwaka 2011 jipange upya kwa kuijua thamani yako ni nini mbele ya jamii na nini makusudio ya Mungu kukuumba mwanamke au mwanaume.
Ukishaijua thamani yako, hapo utajua thamani yako haipo kwa mtu mmoja bali kwa watu wote. Kupendana na kuachana kulikuwepo toka zamani japo kwa ghafla mshtuko wake ni mkubwa.
Lakini linapokutokea ni wakati wa kukaa chini na kutafakali na kujiuliza ni wapi ulipojikwaa ili usirudie makosa ya mwaka uliopita ambao kwako uliona ni mwaka wa nuksi.
Siku zote mwanadamu mwenye akili timamu huwa harudii makosa mara mbili, hasa kwa jambo lililomuumiza. Hii itakusaidia kujua nani mwenye makosa ni wewe au mwenzako.
Kama ni mwenzako ni muda muafaka wa kujitambua una muhimu gani katika dunia hii. Ni kujiamini na kuona kuachwa au kutendwa si mwisho wa kupenda au kupendwa ni kujipanga upya, hakika kila jambo linalochukua muda kulifikili huwa na mafakinio nakutakia mwaka mwema wenye furaha.
Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment