Advertisements

Saturday, January 15, 2011

Mungu amenipa nafasi ya pili

Okoka Sanga
Okoka Sanga ni mtoto wa mchungaji Hossiana Sanga,mchungaji wa kanisa la Lutheran Wilayani Makete,Mkoani Iringa.Okoka Sanga alizaliwa 1968,Makete,mkoani Iringa akiwa mtoto wa 8 kati ya watoto 10 wa Mchungaji Hossiana Sanga.

Okoka Sanga baada ya kumaliza masomo katika Secondary ya Njombe,alienda chuo cha uwalimu Korogwe na baadae alianza kazi ya uwalimu katika shule ya Morogoro secondary mwaka 1993,ambako alifundisha kwa mwaka mmoja na kuhamia Mikumi Lodge mwaka 1994 ambako pia alifanya kazi muda wa mwaka.

Mwaka 1995 alihamia Dar es Salaam na kupata kazi kwenye Hotel ya  Sheraton,hapa alifanya kazi kwa miaka 5,ndipo siku moja alikuja mfanyakazi wa World Bank akitokea Washington,DC,anayeitwa Sati Achath aliyefikia Hotelini hapo na kutokea kumtunuku Sanga na siku aliyokaribia kuondoka alimuuliza Sanga kama kuna kitu anaweza kusaidia.
Okoka Sanga akiwa amelazwa ICU Washigton Hospital Center baada ya kupata ajali mbaya sana ambayo ingeweza kuchukua uhai wake.

OKoka Sanga akamweleza kwamba alikua anamipango ya kwenda kusoma Uingereza,Sati Achath hakupendelea sana wazo la Sanga kwenda Uingereza kusoma ndipo alipomshawishi kama angependelea aje Marekani kusoma kwa sababu Marekani ni"Land Of Oportunity".

Okoka Sanga akiwa ICU Washington Hospital Center 

Ndipo mwaka 2001 Okoka Sanga aliingia Marekani kwa mara ya kwanza na kuanza masomo Strayer University akisomea Bussiness administration na baadae kupata kazi ESPN ZONE.

Mwaka 2005 Okoka Sanga alipata ajali mbaya sana ya gari,mpaka leo hakumbuki nani aliyemgonga anachokumbuka ni jamaa alipita kwenye taa nyekundu na kumgonga ubavuni upande wa dereva na Sanga akapoteza fahamu hapo hapo na jamaa akakimbia na hajaweza kupatikana mpaka leo na gari halijulikani ni la nani kwa sabau halikua na Vin # wala Registration inasemekana gari lilikua la wizi.

Hii ndio gari alilokua akiendesha Okoka Sanga angalia mwenyewe hii ndio inapelekea yeye kusema Mungu amempa nafasi ya pili kuishi.

Hali aliyokua nayo Sanga ilibidi akimbizwe hospitalini na Helcopter ili kuokoa maisha yake,Madaktari walivyomuana walimpeleka moja kwa moja ICU kwani alikua kwenye koma na alikaa ICU kwa wiki mbili na wiki ya tatu fahamu zilianza kurudi.

Kutokana na hali aliyokuwa nayo,Daktari Bingwa wa Washington Hospital Center,alitegemea Sanga angeendelea kuwepo hospitalini hapo kwa mwaka mmoja  na hii nikutokana na tone la damu kuvilia kwenye ubongo.Lakini kwa maajabu yake Mwenyezi Mungu,Sanga alikaa kwa muda wa mwezi mmoja mpaka Daktari Bingwa kushangazwa na kudiriki kumuuliza kwanini anapona haraka namna hiyo,Sanga hakua na cha kumjibu zaidi ya kusema moyoni"Mwenyezi Mungu ananipa nafasi ya pili ya kuishi"
Gari la Sanga likiwa nyang'anyang'a

Okoka Sanga baada ya kukaa wiki mbili akiwa kwenye koma hospitalini hapo na alipozinduka,akili ikawa haikumbuki chochote maskini akaanza upya kama mtoto mdogo kufundishwa kila kitu kuongea,kuandika,kutembea,kula na mambo mengine mengi ambayo yote haya yalifanyikia Rehabilitation(mama cheza)
Okoka Sanga alikua hawezi kuongea mawasiliano pekee ilikua ni kumwandikia kama unavyoona hapa mtu akamuulia unajisikiaje lakini yeye alimjibu anaendelea vizuri kwa kua akili ilikua imekufa hata kuandika kulimshinda.

Kusema ukweli maisha ya Sanga ni kama kuzaliwa upya ndio maana yeye anayaita"Mungu amenipa nafasi ya pili",laiti angejua yote haya pengine huku Marekani asingekuja lakini yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu.
Hapa Sanga anaulizwa wapi panauma lakini masikini kuandika hawezi tena anachora kama mtoto aliyeanza kutambaa.

Okoka Sanga hakukaa Hospitali muda mrefu hii ilishangaza madaktari lakini yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu,aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya mwezi mmoja na alikaa nyumba kwa siku 30 kabla hajarudi kazini wakati huu alikua bado anafanya kazi na ESPN ZONE,chakuchekesha wafanyakazi wenzake walikua wanaogopa kum-hug wakifikiria watamuumiza.

Gharama za hospitali zilifikia $211,000 na Insurance walimlipia $190,000.

Kwa sasa Okoka Sanga amepona kabisa na anaendelea na shughuli za kila siku kama binadamu mwingine wa kawaida na sasa anajishughulisha na kutengeneza kadi zenye picha za wanyama mbali mbali wanaopatikana Tanzania kwenye mbuga zetu,mlima Kilimanjaro,maeneo muhimu yanayowavutia watalii kama vile soko la watumwa Zanzibar.
Hii scarf ni moja zawadi aliyopewa na Msauzi Hans Burger

Wazo lakuanzisha bishara hii alilipata alipokutana na pilot wa South Africa Airways miaka miwili kabla ya kombe la dunia ambalo mwaka jana South Africa walikua wenyeji.

Bwana Hans Burger aliporudi kwao alimtumia Scarf na kadi yenye picha za wanyama,ile kadi ilimfumbua macho ndipo akaanzisha biashara hiyo lakini yeye akitumia picha za vivutio vya kitalii kutoka Tanzania.
Na Balozi zetu Washington,DC na New York wamemuunga mkono kwa kutumia kadi zake wakati wa sikukuu ya Xmas na mwaka mpya kuwatumia Balozi zingine na sehemu mbali mbali za serikali ya Marekani,kusema ukweli tunawapongeza sana kwa kuthamini kazi za wajasili mali wanaoishi ughaibuni.

Sanga ametengeneza Kalenda yenye picha ya mlima Kilimanjaro na upande wa chini kulia unaonyesha sikukuu zote za Marekani na kushoto inaonyesha sikukuu zote Tanzania. Kalenda hizi ataziuza kwa ajili ya charity na pesa zitakazopatikana atazipeleka Makete,mkoani Iringa kwa ajili ya kusaidia watoto yatima,amesema kwa sasa anahitaji apate kama $1,000 yakuanzia ili kusaidia kuwasomesha watoto yatima hao ambao wazazi wao wamekufa kwa ukimwi.
Kalenda zinazouzwa ilikuchangisha pesa za kuwasaidia watoto yatima Makete

Amesema zamani alikua akimpelekea baba yake pesa lakini alishangaa baada ya siku chache pesa imeisha,alipomuuliza baba vipi pesa unafanyia nini ndipo baba yake alipomuambia "mwanangu nawasaidia hawa watoto yatima inasikitisha kuona mtoto analea mtoto mwenzie na kua mkuu wa familia".Sanga aliingiwa na imani na ndipo alipokuja na wazo la kutengezeza kalenda ili mauzo yake yatumike kusadia kusomesha watoto hao.

Okoka Sanga kwa sasa anaishi Washington,DC,anafanyakazi na kuendesha shughuli zake mwenyewe

Wadau wa Vijimambo Sanga anaomba Sapoti yenu ya kununua kalenda kwa wingi  ili tuwasaidie watoto wa Makete na wengineo Tanzania.

Kalenda zinapatikana 
Tecla Mwesiumu Kessy,Baltimore,443-518-6448
Okoka Sanga,Silver Spring,240-505-7280
Peninah Mshiu,San Fransisco,CA,415-901-4449

Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania. 

3 comments:

Anonymous said...

Oh! How amazing!
The article moves the mind while beating the senses on how life can be transformed.
We will be there brother to support your mission!
May God Bless you!

Edward Emmanuel

Anonymous said...

Your article is so touchy!
We thank the Almighty God for miraculously enabling us to have you for the second time.
This teaches us that God has his own purposes to his people.

Please, know that we are here for you.

with love,
Agatha Nyundo

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu akubariki kaka.Tunaweza kaa chini na kumpangia mwenyezi Mungu but he has better plans for us way beyond our imagination.
sheila.