Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameahidi kutoa kiasi cha Sh 5 milioni kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa kompyuta 24 zinazohitajika katika kituo cha kulea watoto yatima cha SOS kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu jana ilieleza kuwa Pinda alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea kituo hicho kukagua madarasa ya shule hiyo ya awali pamoja na nyumba wanazoishi watoto hao.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Pinda alitoa mchango huo baada ya kuelezwa kuwa kituo hicho kina mpango wa kuanzisha darasa maalumu la kompyuta ili watoto hao waweze kupata mafunzo ya teknolojia ya habari (IT) na kwamba kituo kinahitaji kompyuta 24.
Ilieleza kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho, Dk Alex Lengeju alimweleza Waziri Mkuu kwamba kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji 500 vya SOS vya kulea watoto yatima vilivyopo katika nchi mbalimbali duniani ambavyo vinatumia mfumo wa familia mbadala.
“Inaumiza kuona watoto wakiishia mitaani, tunachofanya ni kuwachukua watoto ambao hawana ndugu na tunawalea, hapa wanaishi watoto 10 katika nyumba moja chini ya uangalizi wa mlezi ambaye ndiye mama wa familia hiyo,” ilieleza taarifa hiyo,
“Tunawalea hivyo ili watambue mfumo wa kuishi kama familia na kuishi kama wanakijiji wakitambua uwepo wa majirani zao,” ilieleza taarifa hiyo ikimnukuu Lengeju.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kijiji hicho kina nyumba 13 zenye uwezo wa kuchukua watoto 130 ambapo hadi sasa kina watoto 123 ambao wanasoma shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam huku wengi wao wakiwa shule ya awali iliyopo ndani ya kijiji hicho.
Ilieleza kuwa kijiji cha SOS kimeanzisha pia mpango wa kuimarisha familia kwa kutoa huduma kwa walengwa wanaoishi nje ya kituo hicho kwa kuwalisha, kuwaelimisha na kuwaandaa wajitegemee kimaisha na kwamba hadi sasa wanahudumia watoto 200 na watoa huduma 53.
Ilifafanua kuwa kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo kwenye jamii, wana mpango wa kuhudumia watoto 1,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment