![]() | |
|
Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Mkuu wa Polisi, (IGP) Said Mwema, alisema amezuia maandamano hayo baada ya kupata taarifa za kiintelejinsia kuwa yangesababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Alisema kabla ya uamuzi huo, Chadema iliomba kibali cha kufanya maandamano na mkutano huo leo na kuruhusiwa lakini baada ya uchunguzi ameamua kuzuia maandamano hayo ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kujitokeza.
“Polisi inaendelea kukusanya taarifa za tishio hilo na mengineyo yanayohatarisha uvunjifu wa amani na yanayofanana na hayo kwa lengo la kuhakikisha utulivu kwa wananchi wote unakuwepo,” alisema IGP Mwema.
Alifafanua kuwa Polisi haina nia ya kuzuia kufanyika kwa maandamano ya aina yoyote, kwa kuwa yapo halali kisheria lakini uamuzi huo unatokana na dalili za kutokea kwa fujo.
Alisema pamoja na kuruhusu mkutano huo, Polisi itaimarisha ulinzi wa kutosha tofauti na kawaida ili kuhakikisha utulivu na amani vinatawala wakati wote wa mkutano huo.
“Tunawaomba wazazi wasiruhusu watoto wao kuingia katika mikusanyiko mitaani ambayo kimsingi inaweza ikawaletea madhara kutokana na hali iliyopo kwa sasa wakati huu ambao kuna tishio, bado tunaendelea kufuatilia kujua undani wake,”alisema IGP Mwema.

No comments:
Post a Comment