ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 17, 2011

Usiuchezee moyo sebene, lazimisha hisia, nyenyekea

Ni mwaka mpya wa 2011, inakubidi na wewe uwe na fikra mpya.
Uondokane na vitu ambavyo vinaweza kukuondolea mvuto au kukuingiza kwenye migogoro. Jiepushe na kila kilichokugombanisha na mwenzi wako.


Ni vizuri uwe na hisia hizo ili somo hili likuingie sawia. Mapenzi hayahitaji ugumu. Huwezi kusifiwa kwa kushindwa kumnyenyekea mwenzi wako. Jeuri dhidi ya mwenzako, maana yake una alama ‘F’ kwenye mapenzi.

Kila mtu anapenda kuonewa wivu ili awe na uthibitisho kuhusu mvuto wake. Anahitaji kujua kama anapendwa na kwamba yupo anayemjali, kwa hiyo asipokuwa karibu yake, atamsumbua kwa maswali; “Uko wapi? Unafanya nini? Na nani?”

Asije kukudanganya mtu kuwa hapendi kuonewa wivu. Nimelazimika kutoa neno hili kwa sababu kumekuwa na tabia ya watu kuongopeana kuwa hawapendi usumbufu. Wengine wanajaza hekima dhaifu za mapokeo ya kizamani: “Mimi mpenzi wangu mzungu, hanibani wala nini!”

Je, ni kweli kuwa wazungu hawana wivu? Unajua ni kwa nini Chris Brown alimpa kipigo Robyn Rihanna Fenty? Uhusiano wa kimapenzi una nguzo zake. Moja kati ya nguzo hizo ni jinsi wewe unavyomjali mwenzi wako na kumfanya ajione mwenye thamani.

Hujui kuwa mpenzi ni mali yenye thamani? Kama unatambua hilo ni vizuri kumlinda kwa gharama yoyote. Abiria anahimizwa achunge mzigo wake, iweje wewe usidhamirie kumhifadhi mwandani wako? Akili itulie kichwani kwako, wapo wanaolia kwa kuzidiwa kete na marafiki zao.

Hawajui kuwa walicheza ‘faulo’ ndiyo maana wakajikuta wanawekwa pembeni. Hutaki kumuonesha kuwa unamjali kwa kipimo kinachostahili, matokeo yake rafiki yako anachukua nafasi. Hujui kumuuliza kulikoni anapokuwa mnyonge, mwenzako anatimiza hilo.

Mapenzi ni sanaa ambayo inamtaka mtu aishi ndani ya mwenzi wake. Uwe mwepesi wa kujua yaliyomo kwenye fikra zake. Katika ‘malavidavi’ epuka usistaduu, ubrazameni au ugumu. Unahitaji kuwa rahisi kwa mwenzi wako na kumfanya ajione hajakamilika bila uwepo wako.

Unaweza kufanya kitu ambacho wewe utakiona ni kidogo lakini kwa mwenzako kikawa kimemmaliza kabisa. Fikiria unaamka asubuhi na mapema kisha unamuamsha awahi kazini. Anakuta umemuandalia kila kitu, mnakwenda kuoga pamoja, mnapata kifungua kinywa mezani halafu mnatengana kwa muda kwa sababu mnawajibika ofisi tofauti.

Siyo kwa kuangalia jinsia. Fikiria pia wewe ni mwanaume ambaye unafanya kitu kumfurahisha mwenzi wako. Unaamka mapema na kunyoosha nguo za mkeo. Unamuamsha na anakuta kila kitu kipo tayari, anajiona mwepesi. Anakukumbatia na kukushukuru kwa sababu anakuona ni mtu wa kipekee. Wengi wamelemazwa na mfumo dume!

Kufanya hivyo, haina maana ni ‘ubushoke’ kama inavyoweza kutafsiriwa, isipokuwa ni njia ya kumpa sababu ya kukupenda. Atakuona ni mwanaume bora uliyekamilika, na usipokuwa naye ataona kuna upungufu mkubwa. Usisome kama mapitio ya vitu rahisi, ila unatakiwa kutunza kichwani na kuhamishia katika vitendo kile ambacho unakipata hapa.

Asilimia kubwa ya watu waliosalitiwa kimapenzi na marafiki zao, waliponzwa na tabia ya kutoheshimu hisia za wenzi wao. Kiasili, kuna mambo ambayo mtu anayahitaji kutoka moyoni afanyiwe na mwenzi wake lakini anakuwa hapati hivyo kusababisha aone pengine jirani anaweza kumtekelezea.

CHUKUA MFANO HUU
Justin na Jamie wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitatu sasa. Tatizo kubwa linalowakabili ni kwamba mara kwa mara huwa wanagombana na kusalitiana. Hata hivyo, wao hawajui.

Justin anasema: “Nampenda sana Jamie lakini kuna mambo huwa hanitekelezei, na zaidi huwa nashangaa hata hanionei wivu. Nikiwaona marafiki zangu jinsi wao na wapenzi wao wanavyoishi, nashangaa kwangu mbona haiwi hivyo? Naweza kuwa mbali naye hata kwa siku mbili lakini wala hashtuki, haniulizi.

“Tukikutana haoneshi shauku ya kuwa na mimi mpaka nahisi thamani yangu kwake ni ndogo. Hajawahi hata kunikumbatia na hasemi kama alikuwa amenimisi. Nyumbani kwangu naishi peke yangu lakini hutomsikia akisema anataka kuja mpaka nimuombe, tena kwa kumbembeleza, wakati mwingine anasema yupo bize.

“Tukiwa katika ulingo wa mapenzi haoneshi msisimko. Nijuavyo mimi wanawake wengine hutoa hamasa kwa kuangusha kilio fulani cha mahaba na kusifia jinsi kazi inavyofanyika, Jamie yeye habari hiyo hana. Hata nyonga yake anaibania. Ukimuuliza kama anatosheka anadai anafika bila wasiwasi. Hapa ndipo anaponifanya nijiulize maswali mengi.

“Mara mbili nimejikuta nikitoka na rafiki zake wawili. Wa kwanza alionesha ananijali kuliko hata Jamie mwenyewe. Nilipotoka naye nilijiona mwanaume kamili hasa. Ananiuliza maswali ya mahaba, ananikumbatia kwa bashasha kila tunapokutana. Tukiwa kwenye shughuli ananionesha jinsi anavyoridhika na mimi.

“Mwingine hivyo hivyo, tunapomaliza mchezo ananimwagia sifa kemkemu, ananiambia hajapata mwanaume aliyemsafirisha kule ambako nimempeleka. Katikati ya mahaba ananililia kwa sauti fulani ya kutoka puani. Kusema ukweli, hao marafiki wamenikosha kiasi ambacho naona thamani yao ni kubwa kuliko Jamie.

“Vile vilio vya kimahaba, sauti za kubembeleza na pongezi baada ya kazi ni kitu kikubwa kwangu. Hata kama ni sifa za uongo lakini mimi zinanipeleka pale ninapopataka.

Sijisikii kwenda faragha na mtu ambaye mimi najitahidi kumfurahisha na kumridhisha lakini yeye ananitolea macho utadhani hana hisia. Najisikia kumchoka!”

Itaendelea wiki ijayo...

No comments: