
Wagombea wa kiti cha urais na ubunge nchini Uganda, wanatarajiwa kukamilisha kampeini zao hii leo tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanmyika siku ya Ijumaa.
Rais Yoweri Museveni, ambaye anawania muhula wa nne kama rais wa Uganda, kupitia chama tawala cha national Resistance Movement, NRM, anatarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari leo asubuhi, kabla ya kukamilisha kampeini yake na mkutano wa hadhara mjini Kampala.
Mpinzani mkuu wa rais Museveni, Kizza Besigye anayewania kiti hicho kupitia chama cha Forum for Democratic Change, FDC, naye atakuwa na mkutano katika chuo kikuu kimoja mjini Kampala.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Badru Kiggundu, ametoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya kisiasa nchini humo, kuvunja makundi yote ya wapiganaji ambayo yaliundwa kwa dhamira ya kulinda masanduki ya kupigia kura.
No comments:
Post a Comment