
Wahamiaji haramu 50 raia wa Somalia wanahofiwa kufariki dunia, baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Mozambique siku 10 zilizopita.
Msemaji wa polisi nchini Mozambique, amethibitisha kuwa naodha wa meli hiyo ya Tanzania ni miongoni mwa waliozama katika kisiwa cha Suhavo Kaskazini ma nchi hiyo.
Wahamiaji wengine 80 kutoka mataifa ya Somalia na Ethiopia walionusirika ajali hiyo wamepelekwa katika kambi moja ya wakimbizi katika mkoa wa Nampula nchini humo.
Waandishi wa habari wanasema Mozambique imekuwa njia muhimu kwa wahamiaji haramu wanaotoka mataifa ya Somalia, India na China kuelekea nchini afrika kusini.
No comments:
Post a Comment