ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 12, 2011

LADY IN RED YAFANA

Mwanamuzi wa kizazi kipya, Baby Joseph ‘Madaha’ akifanya makamuzi katika maonesha hayo.
ONYESHO la mavazi la Lady in Red lililoandaliwa na mdau mkubwa wa mambo ya mavazi nchini, Asia Idarous, kupitia kampuni yake ya Fabak Fashion,  usiku wa kuamkia leo, lilifana vilivyo ndani ya Ukumbi wa Hotel ya Movien Pick, ambapo mastaa kibao walihudhulia kushuhudia jinsi mchakato ulivyokwenda.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

Baadhi ya mashabiki wa onesho hilo wakishuhudia mchakato mzima ulivyokuwa.
Muigizaji wa filamu Bongo, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ akishuhudia maonyesho hayo akiwa na bosi wake.
Mmoja wa wanamitindo Reah Mtula (katikati), akifuatilia mchakato huo na Mmbunifu wa mavazi Hadija Mwanamboka (kulia), kushoto ni rafiki yao ambaye jina lake halikuweza kifahamika mara moja.
Mmoja wa wanamitindo akiwa jukwaani tayari kwa kuonyesha vazi lake.
Mwanamitindo maarufu nchini Fideline Iranga (katikati), akiwa na marafiki zake.
Muandaaji wa shughuli hiyo, Asia Idarous na mumewe (wa pili katikati), akiwapungia mkono wa pongeziwote waliohudhuria ishu hiyo, wengine ni baadhi ya wanamitindo wake.
Miss Progress Julieth Wiliam, akikabidhiwa cheti na mmoja wa wabunifu wa mavazi Peter Mwendapole, kulia ni mushereheshaji wa shughuli hiyo, Jokate Mwegelo.
Baadhi ya wanamitindo wakiwa kwenye pozi la pamoja.
MC Jokate Mwegelo akiwa kwenye pozi muda mfupi baada ya kuhitimisha shughuli hiyo.

Picha: Musa Mateja/GPL

No comments: