ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 24, 2011

Mume, mke wauawa kwa tuhuma za uchawi

MTU na mkewe wakazi wa kijiji cha Itenka wilayani Mpanda wameuawa kwa kukatwa na mapanga na watu wasiofahamika wakiwashutumu kuwaua kwa kuwaroga wajawazito na watoto wadogo kwa ajili ya kujitajirisha kupitia uchimbaji wa dhahabu. 


Wanandoa hao, Henci Mponya (45) na mkewe, Kangwa Nzemo (38) ambao ni wachimbaji wadogo wa dhahabu kijijini humo, wameuawa jana. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage amethibitisha kuwapo mauaji hayo yaliyofanywa saa 7 usiku baada ya wavamizi kuvunja mlango wakati wanandoa hao wakiwa wamelala nyumbani. 

Taarifa zilizopatikana ni kwamba walikuwa wakishutumiwa kwa muda mrefu na wanakijiji kusababishia vifo vya wajawazito na watoto wadogo na kuharibu kichawi mimba kwa lengo la kuwawezesha kupata dhahabu nyingi wanapochimba madini kwenye mashimo yao. 

Inadaiwa kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wanandoa hao kwenda kwenye nyumba ya jirani yao aliyekuwa mjamzito na kula naye chakula kisha kufunga mabaki kwenye kitambaa na kwenda nayo kwenye mashimbo yao na kufanya matambiko. 

Inadaiwa mama huyo alikufa ghafla siku iliyofuata. Kwa mujibu wa Kamanda Matange, wanandoa Walivuja damu nyingi na kufa papo hapo huku wahusika wakiwa wametoweka. 

Mantage alisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini wauaji ili wakamatwe.


CHANZO:HABRI LEO

No comments: