meandikwa na Mwandishi,
IDARA ya Vitambulisho vya Taifa Zanzibar (Zan ID) imetangazwa kuwa mshindi wa kutengeneza vitambulisho bora vinavyokidhi viwango vya kimataifa kutokana na vigezo vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
“Cheti hiki ni kutambua uwezo wetu wa kuzalisha vitambulisho vyenye viwango bora na tumedhamiria kuwapa wateja wetu bidhaa bora zaidi na serikali inatuunga mkono katika hilo,” alisema Mkurugenzi wa Zan ID Mohamed Ame kabla ya kupokea cheti hicho kutoka kwa
wakaguzi wa ISO.
IDARA ya Vitambulisho vya Taifa Zanzibar (Zan ID) imetangazwa kuwa mshindi wa kutengeneza vitambulisho bora vinavyokidhi viwango vya kimataifa kutokana na vigezo vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
“Cheti hiki ni kutambua uwezo wetu wa kuzalisha vitambulisho vyenye viwango bora na tumedhamiria kuwapa wateja wetu bidhaa bora zaidi na serikali inatuunga mkono katika hilo,” alisema Mkurugenzi wa Zan ID Mohamed Ame kabla ya kupokea cheti hicho kutoka kwa
wakaguzi wa ISO.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika mjini hapa, alisema Wazanzibari 645,000 tayari wameshapatiwa vitambulisho vya taifa.
Kutokana na hatua hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Baraza la Mapinduzi, Dk. Mwinyihaji Haji Makame aliipongeza idara hiyo kwa kazi nzuri.
“Kutambuliwa kimataifa ni jambo la kujivunia! Sasa tumedhamiria pia kuboresha huduma zetu za teknolojia ya habari,” alisema Dk. Mwinyihaji.
Hii ni mara ya tano kwa Zan ID kupata cheti cha ISO 27001 na 9001 hali itakayosaidia kuzivutia baadhi ya nchi kwenda kujifunza kwa idara hiyo jinsi ya kuboresha bidhaa zao ziwe bora na vikubaliwe katika viwango vya kimataifa.
Akikabidhi cheti hicho, Mtaalamu kutoka Israel, Meray Vered ambaye ni Makamu Rais wa Idara ya Usalama ya Kimataifa pamoja na Avraham Rost ambaye ni Mkaguzi wa Viwango katika Taasisi ya Viwango vya Israel (SII), walisema Idara ya Vitambulisho Zanzibar
inatumia teknolojia ya kisasa na inayokubalika kimataifa.
“Amini usiamini nchi yangu sasa ndio inaondoa teknolojia ya kizamani ambayo tulikuwa tunatumia ili iweze kutumia teknolojia hii inayotumiwa na idara ya vitambulisho ya Zanzibar,” alisema Rost.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Zan ID, nchi jirani kama Uganda, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya Muungano tayari zimeshaenda kujifunza teknolojia hiyo ili waitumie katika mpango wa kutengeneza vitambulisho vya taifa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais wa Zanzibar (Ikulu) Dk. Mwinyijaji Makame (katikati) akionyesha shahada ya ubora wa vitambulisho kwa afisi ya vitambulisho Zanzibar baada ya kukaguliwa na Mkaguzi Kiongozi, Avraham Rost kutoka taasisi ya kimataifa ya Standards Institution ya Israel (SII) sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View jana. Kulia ni Mkurugenzi wa vitambulisho vya Mzanzibari, Mohamed Juma Ame. Picha na Martin Kabemba.Waziri wa Nchi ofisi ya Rais wa Zanzibar (Ikulu) Dk. Mwinyijaji Makame (katikati) akionyesha shahada ya ubora wa vitambulisho kwa afisi ya vitambulisho Zanzibar baada ya kukaguliwa na Mkaguzi Kiongozi, Avraham Rost kutoka taasisi ya kimataifa ya Standards Institution ya Israel (SII) sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View jana. Kulia ni Mkurugenzi wa vitambulisho vya Mzanzibari, Mohamed Juma Ame. Picha na Martin Kabemba.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Ikulu), Dk. Mwinyihaji Makame (kulia) na Mkaguzi kiongozi wa ubora wa vitambulisho vya Mzanzibari kutoka Standards Institution ya Israel, Avraham Rost wakionyesha shahada zilizotolewa kwa ofisi ya vitambulisho Zanzibar jana kwenye sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View. Picha na Martin Kabemba
No comments:
Post a Comment