
Na Mwandishi Wetu, Congo DR
WACHEZAJI wa Simba wameyatema mamilioni waliyoahidiwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa bingwa mtetezi, TP Mazembe katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika jana kwenye Uwanja wa Kenya, jijini Lubumbashi Congo DR.
WACHEZAJI wa Simba wameyatema mamilioni waliyoahidiwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa bingwa mtetezi, TP Mazembe katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika jana kwenye Uwanja wa Kenya, jijini Lubumbashi Congo DR.
Kwa matokeo hayo, ili Simba iliyorejea nchini jana saa 4:00 usiku iweze kusonga mbele katika michuano hiyo na kuivua ubingwa Mazembe, inatakiwa kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Simba uliahidi kutoa Sh milioni 100 kwa wachezaji wa timu hiyo kama wakishinda mchezo huo na milioni 50 kama wangemaliza mchezo huo kwa sare, lakini mambo hayakuwa kama walivyopanga.
Simba walianza mchezo huo kwa kasi huku wakicheza mpira wa kujiamini lakini walijikuta wakifungwa bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Patou Kabangu kwa shuti kali la mbali ambalo lilimshinda kipa Juma Kaseja.
Mazembe waliendelea kulisakama lango la Simba ambao walionyesha kujilinda zaidi na kupata bao la pili dakika ya 24 mfungaji akiwa Narlise Ekanga akimalizia pasi nzuri ya Alain Kaluyitika aliyeingia ndani ya eneo la hatari huku mabeki wakidhani ameotea.
Kipindi cha pili Mazembe walianza kwa kasi iliyozaa matunda dakika ya 64 kupitia kwa Kaluyitika baada ya kuipangua ngome ya Simba na kuachia shuti lililomshinda Kaseja na kujaa wavuni.
Simba, mabingwa hao wa Tanzania Bara hawakukata tamaa ya kusaka bao na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 76 lililofungwa na Emmanuel Okwi kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani eneo la hatari na kipa wa Mazembe Robert Kidiaba akiwa katika harakati za kufunga.
No comments:
Post a Comment