
Lila Hussein (24 pichani), aliyechomwa moto na Mkurugenzi wa Hoteli ya kitalii ya South Beach, iliyoko Kigamboni Mjimwema, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, amekufa usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa akiuguza majeraha.
Mkurugenzi aliyedaiwa kufanya unyama huo, Salim Noto (53), anashikiliwa na polisi.
Hussein, alikufa saa 7:30 usiku wa kuamkia jana hospitalini hapo alipokuwa amelazwa tangu Aprili 9, mwaka huu akiuguza majeraha ya moto huo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi David Misime, alilithibitishia NIPASHE kwamba alipokea taarifa za kifo cha Hussein mapema jana asubuhi.
Kamanda Misime alisema polisi tayari wanawashikilia watuhumiwa wawili, Noto na John Mangiombi na watafikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya mauaji.
"Ni kweli Hussein amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (jana) na tayari tunawashikilia watuhumiwa wawili ambao kesho (leo), watafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji," alisema Kamanda Misime.
Awali, Noto kwa kushirikiana na wenzake wawili, Meneja wa hoteli hiyo, mwenye asili ya Kiasia, Salim Nassoro (20), mkazi wa Mjimwema, na dereva, Mwangiombi (32), mkazi wa Mikocheni, jijini Dar es Salaam, walidaiwa kumchoma moto Hussein na kusababisha kifo chake.
Ilidaiwa kuwa watu hao walimvisha kijana huyo gurudumu la gari na kummwagia petroli mwilini na kisha kumchoma moto kwa kibiriti.
Alisema baada ya tukio hilo, alipelekwa katika kituo cha afya Kigamboni akitokea kituo cha polisi cha Mjimwema na baadaye akahamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Taarifa zilizopatikana maeneo hayo zilisema kuwa marehemu alichomwa moto kwa madai ya kuingia bila kulipa kiingilio kwenye muziki wa disko uliokuwa ukipigwa katika hoteli hiyo.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Hivi baadhi ya wa-Asia bado wana jeuri Bongo huh?
Hivi hicho kiingilio cha disco kilikuwa ni shilingi ngapi mpaka wamuue mbongo kwa kumchoma moto?
Je sheria zitachukuwa mkondo weke au ni yale yale sheria haziwahusu wenye pesa? Ni unyama mkubwa sana huu. Wahusika wa vyombo vya sheria waangalie maswala kama haya dunia ya sasa watu wana hasira wanaweza kuanza kuwang'ania wauaji na wanyanyasaji wa wabongo ukizingatia mgeni anajifanya ana mbegu kubwa zinazoning'inia na mbabe kwetu.
Naomba rais Jakaya Kikwete aingilie swala hili kama rais wetu ajaribu kuwaa "clue in" kuwa wanajijengea uhusiano mbaya na Watanzania ambayo ni wakarimu. Huu ni uchokozi wa waziwazi kabisa. Pia wabongo wenzangu naomba kuliangalia hili swala.
Ndugu yako kachomwa moto na kuporwa uhai wake kwa kuliingili cha chini ya $100 ya Kimarekani wewe ungejisikiage na ungefanya nini kama vyombo husika havitaichukulia hii kesi kama mfano kwa watu/wageni na wengine wanaochukuwa sheria mikononi kwao. Kwanza hii ni dharau kwa jamii ya watanzania wenye kuthamini maisha/uhai wa kila mmoja.
Nadhani upo haja na wengine kuchukua sheria mikononi kwa watu kama huyo anayejisikia kama anapesa ambazo kuna uwezekano mkubwa amezipatia hapo bongo kwa kupewa nafasi ya kuishi hapo.
Kabla sijapandwa na hasira naomba watanzania mchangie hili swala
Post a Comment