Advertisements

Friday, April 29, 2011

Bafana Bafana kucheza na Stars May 14,2011

iol spt apr29 Bafana
Bafana Bafana itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Tanzania(Taifa Stars) mjini Dar May 14,2011,Chama cha mpira a miguu cha Afrika ya kusini(SAFA) kimethibitisha kuwepo kwa mchezo huo.

Mwenyekiti wa SAFA Pinky Lehoko,amesema kimsingi makubaliano ya kuwepo kwa mechi hiyo yameishafikiwa,na chama cha mpira wa miguu Duniani (FIFA)wameishaiweka mechi hiyo kwenye ratiba.

Timu ya Bafana Bafana ni ya 39 kwa ubora wa mpira wa miguu Duniani na Taifa Stars ni ya 123.

Kocha wa Bafana Bafana Pitso Mosimane anatarajia kutangaza kikosi chake wiki ijayo,kikosi hiki hakitawajumuisha wachezaji wa timu ya Orlando Pirates kwa sababu watakua wanacheza nusu fainali ya kombe la Nedbank wiki hiyo hiyo ya mechi ya Stars na Bafana Bafana.

Mechi hii itakuwa ya mwisho kwa Bafana Bafana ya kujipima nguvu kabla ya timu haijaelekea Misri June 3,2011 kucheza mechi ya kundi G 2012 ya Africa Cup of Nations Qualifier dhidi ya Misri.

Afrika Kusini ndio inayoongoza kundi hiliokwa kufikisha  pointi saba kwa kucheza mechi tatu, kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.


No comments: