ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 22, 2011

FASHION RUNAWAY SATURDAY APRIL 23,2011

New England Umoja inawaletea maonyesho ya mavazi ya kwanza na ya kipekee ya Ki-Tanzania
yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii tarehe 23, 2011 Katika ukumbi wa KNIGHT OF COLUMBUS 484 Lancaster st,MA 01453. Maonyesho hayo kabambe yataanza saa mbili usiku kwa Chakula cha Jioni (Dinner).
"Fashion Show" itaanza Saa 4 Kamili Usiku, na Muziki utafuatia mpaka saa saba usiku. Kiingilio $15 kwa watu wazima na watoto $5.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Mama Maarufu wa mitindo Tanzania "Aunt"
Asia Idarous Hamsini. Ameahidi kutoa burudani ya kupoza Roho!.
Chukuwa tiketi yako mapema kabla hujakosa uhondo!!. Tiketi zipo kwa idadi Maalum. Kwa maelezo
zaidi kuhusu tiketi gonga www.newenglandumoja.net
Maandalizi ya Maonyesho hayo yamekamilika yakiwa na washiriki kutoka pande
mbalimbali za mikoa ya MA,CT,NH,RI,NY,NJ,DC. wamethibitisha kushiriki Maonyesho
hayo ya aina yake. Pia Katika Maonyesho hayo kutakuwa na mgeni kutoka Bongo ambaye alikuwa kwenye fainali
ya Bongo star search "JOSEPH MAIGE" ambae atatoa burudani yake katika jitihada za kuunga mkono N.E.U Foundation.
Burudani ya Muziki pia itatolewa na Ma-DJ wetu Mahiri Rich-Maka na Masudi, na  DJ Mualikwa Kutoka DC, si mwingine isipokuwa DJ Luca ambao kwa pamoja watafanya vitu vyao kama kawaida!.
Mnakaribishwa wote kwenye maonyesho hayo ya aina yake

No comments: