ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 21, 2011

Mama mbaroni kwa kutupa kichanga chooni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
Mkazi wa Mikocheni ‘A’, jijini Dar es Salaam, Happy Fredy (28), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumtupa mtoto mchanga chooni baada ya kujifungua.
Akielezea kitendo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema mwanamke huyo alipojihisi uchungu, alimuomba wifi yake, Shadya Ally, ampeleke hospitali.

Alisema wakiwa njiani, Happy aliingia choo cha jirani kujisaidia, lakini dakika chache baadaye, wifi yake aliyekuwa akimsubiri nje, alisikia sauti ya kichanga akilia.
“Akamfuata humo chooni na kukuta kitoto cha jinsia ya kiume kikiwa pembeni ya tundu la choo,” alisema Kenyela.
Alisema wifi huyo alianza kumulika kwa kutumia simu yake na kumuona Happy akiwa anakisukuma kichanga hicho kwa kutumia mguu ili akitumbukize katika shimo la choo, huku akidai kimeharibika.
Alisema baada ya Happy kukitumbukiza kichanga hicho chooni, Shadya alienda kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay ili kupata msaada zaidi. Alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments: