ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 21, 2011

HAMMIE RAJAB AFARIKI DUNIA!

Habari za kusikitsiha zilizotufikia asubuhi ya leo zinasema kuwa Mzee Hammie Rajab (kwenye kiduara) amefariki dunia katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam alfajiri ya leo, ambako alikuwa amelazwa kutokana na ugonjwa wa malaria. Mzee Hammie, alikuwa ni movie Director, Script writer na mtunzi wa hadithi za vitabu maarufu nchini Tanzania. Moja ya kazi zake maarufu kwa upande wa filamu ni movie ya Tears On Valentine Day, ambayo iko sokoni hivi sasa. Pichani, juu na chini, akiwa kazini aki direct movie hiyo siku za hivi karibuni. Habari zaidi zitawajia baadae.

CHANZO:GPL

No comments: