
AHLANI WASAHLANI
wasomaji wangu wapendwa, leo tena tunakutana katika Mashamsham ili kuweza kupata kile kitu roho inapenda. Najua wengi wenu ni wazima na tayari mmeshaungana nami kupata mwendelezo ulioanza wiki iliyopita.
Naam! Kwanini wanaume wanakuacha mara kwa mara? Hili ndilo swali linalotuongoza katika mada yetu ambayo bila shaka ina maneno mengine yanayoumiza lakini ndiyo dawa inayotakiwa kukubadilisha mtazamo wako.
wasomaji wangu wapendwa, leo tena tunakutana katika Mashamsham ili kuweza kupata kile kitu roho inapenda. Najua wengi wenu ni wazima na tayari mmeshaungana nami kupata mwendelezo ulioanza wiki iliyopita.
Naam! Kwanini wanaume wanakuacha mara kwa mara? Hili ndilo swali linalotuongoza katika mada yetu ambayo bila shaka ina maneno mengine yanayoumiza lakini ndiyo dawa inayotakiwa kukubadilisha mtazamo wako.
Wiki iliyopita nilianza kwa kukupa japo kwa uchache, binafsi naweza kusema kwamba nilitoa ‘First Aid’, leo tiba kamili. Unajua sababu nyingine zaidi? Hebu twende basi tukaone hapo chini.
Unaonesha udhaifu?
Kuna kundi la wanawake ambao hawajiamini kabisa katika maisha yao ya kimapenzi, wana papara na wanasumbuliwa na akili ya kupenda maisha ya haraka.
Kwa kawaida wanawake ni watu wa kutaka vitu kwa haraka sana lakini kwako wewe, si vyema kuionesha haraka yako kwa jamaa uliyekutana naye juzi tu, hasa linapokuja suala la ndoa. Utakuta mwanamke kila mara anamuuliza mwanaume wake: “Baby utanioa kweli?”
Hii inaonesha ni kwa kiasi gani hujiamini na ulivyo muoga na unapenda kuharakisha maisha ili ufiche udhaifu ulionao.
Napenda kukuambia kitu kimoja, wanaume wengi hawapendi kuharakishwa kufanya jambo fulani, si suala la ndoa pekee bali na mengineyo pia.
Wanaume wanapenda kufanya mambo yao taratibu, bila papara wala kulazimishwa. Hujisikia fahari zaidi kama wakifanya jambo kwa mtazamo wao, mara nyingi hupenda kufanya ‘sapraizi’ fulani, siyo kumwendesha kama gari bovu!
Ili kukabiliana na jambo hilo, jiamini na fanya mambo yako kwa uhakika ukimuacha mwanaume mwenyewe aamini kwamba wewe ndiye unayefaa kuwa waziri mkuu wa kuongoza serikali ya moyo wake. Upo rafiki yangu?
KUTOMWAMINI
Umeanza naye uhusino juzi tu lakini umeshaanza kumfuatilia nyendo zake, mbaya zaidi umekuwa mpekepeke wa kuchunguza kila kitu chake.
Mfano umeingia Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) katika simu yake, hukujivunga umeiparamia na kuanza kuusoma ili upate kujua umetoka kwa nani! Hili ni tatizo.
Mwanaume hapendi kuchungwa sana, hata kama hana mambo ya ovyo, lakini atakapogundua kwamba unamfuatilia sana atakuogopa na kubadilisha mawazo.
Unachotakiwa kufanya ni kuonesha utulivu wako na kujenga imani kwa mwenza wako.
Wanaume wengi wanaamini kwamba ukiona mwanamke mpekepeke moja kwa moja ni kwamba hata yeye hajatulia, ana mambo mengi ya ajabu ambayo anayaficha.
ULIMI
Unautumiaje ulimi katika kufikisha ujumbe wako kwa mwanaume ambaye umekutana naye hivi karibuni? Moja kati ya sifa mbaya ya mwanamke ni kuongea sana, haipendezi kuona mwanamke aliyefunzwa akafunzika akawa anaongea kama kasuku.
Wanaume wanapenda mwanamke mwenye haya, anayejua vibaya na asiyekuwa na maneno mabaya katika kinywa chake! Siku si nyingi tangu uanze uhusiano na mwanaume anakubaini kwamba wewe unachonga sana, lazima atakupiga kibuti tu.
Eti marafiki zangu, baada ya kuona yote hayo, kuna sababu ya kuendelea kuachwa na wanaume kila mara? Bila shaka hakuna. Yafuate ili upate mwanaume wa kudumu.
Alamsiki!
Kwa mada nyingine kali tuonane wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment