ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 2, 2011

Mbatia aupinga muswadawa Tume ya Katiba Mpya

Chama cha NCCR-Mageuzi kimepinga muswaada wa katiba wa mwaka 2011 kwa madai kwamba unaonyesha wazi kuwa serikali imepania kumpa Rais mamlaka ya kuunda tume ya kusimamia katiba hiyo, na kwamba mfumo huo umenakiliwa kutoka katika sheria ya Kenya ya marejeo ya katiba yake namba 9 ya mwaka 2008.
Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, alisema jana kuwa mfumo huo unaonyesha kuwa Rais pekee ndiye mdau mkuu katika mchakato wa kutunga sheria.

“Maudhui ya mswaada wa marejeo ya katiba wa mwaka 2011 yanaonyesha kuwa serikali imepania kumpa mamlaka Rais kuunda tume ya kutunga katiba jambo ambalo sio sahihi na hata hivyo mfumo huu umekaliliwa kutoka katika sheria ya Kenya ya marejeo ya katiba namba 9 ya mwaka 2008,” alisema.
Alisema vipo vifungu vingi vyenye kasoro ambavyo vinatoa mamlaka kwa Rais kutawala mchakato wa kutunga katiba.
Alisema baadhi ya vifungu hivyo ni pamoja na kile cha 8 (1) ambacho kinampa mamlaka ya kuipatia tume kuunga hadidu za rejea, kifungu cha 13 (2) kinachomruhusu kuteua katibu wa tume ya katiba na kifungu cha 16(2) kinachoiwajibisha tume kuwasilisha ripoti yake kwa Rais na nakala ya ripoti hiyo kupelekwa na Rais wa Zanzibar.
Aidha alisema kifungu kingine ni kile cha 16 (3) kinachompa Rais wajibu wa kuifanyia kazi ripoti hiyo na kasha kumwamuru Waziri kupeleka muswaada wa katiba mpya katika Bunge la kutunga sheria.
CHANZO: NIPASHE

No comments: