ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 20, 2011

RC atoa upendeleo kwenda kwa Babu

Mchungaji Ambikilile Mwasapila katika kijiji cha Samunge-Loliondo
Mkoa wa Arusha jana uliamua kutotekeleza ahadi ya kusitisha safari za wagonjwa wanaokwenda kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambikilile Mwasapila katika kijiji cha Samunge-Loliondo, wilayani Ngorongoro na kuwaruhusu wagonjwa kutoka mikoa ya mbali kwenda kwa mchungaji huyo.
 

Mchungaji Mwasapila alishatangaza kuwa atasitisha huduma ya tiba kuanzia Ijumaa hadi Jumapatu kwa ajiuli ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.




Juzi, Shirima aliwaambia waandishi wa habari kuwa safari za kwenda Samunge kupata tiba zingesimamishwa kwanzia jana, ili kutoa fursa kwa mchungaji huyo kumaliza kuwapatia tiba idadi kubwa ya wagonjwa waliofurika ghafla siku chache zilizopita na kusababisha  msongamano wa kilomita 25 kutoka kwake.

Jana Shirima aliamuru magari ya abiria kutoka mikoa ya mbali waliokutwa na tangazo la kusitishwa kwa safari za kwenda Samunge wakiwa njiani, waruhusiwe kwenda kupata kikombe.
Shirima aliwataka wahusika wa vituo hivyo husika kuwaruhusu wale wote waliokutwa na tangazo la kusitisha huduma, wakiwa tayari Arusha, waruhusiwe kwenda ili kuepuka malalamiko.


Afisa Habari wa Mkoa wa Arusha, Yotamu Ndenbeka, alisema kuwa Shirima aliziagiza mamlaka husika kuhakikisha zinawaruhusu wagonjwa hao kuondoka na kwamba waliondoka jana alifajiri.


Wakizungumza katika kituo cha kwenda Samunge kilichopo eneo la Kilombero Mjini Arusha, John Jackson, makazi wa Sumbawanga, aliiambia NIPASHE kuwa ameshukuru busara za Shirima kwa kuwaruhusu watu waliotoka mbali kwenda Samunge.

Sisi tumefika hapa Arusha tangu juzi ila kwa sababu tunaruhusiwa kwa awamu ya watu 500, tutafika leo (jana) ila kuanzia jana (juzi) usiku kuna baadhi ya wenzetu wa mikoa ya mbali kama Lindi na Mtwara nao wameruhusiwa kwenda Samunge,” alisema Jackson.

Alisema kuwa jana ilikuwa awamu ya mwisho kuruhusiwa na kuongeza kuwa walielezwa kuwa baada ya hapo hawataruhusu magari mengine kwa sababu wanaohitaji huduma watakuwa wamesikia tangazo la usitishaji huduma hiyo kabla ya kuanza safari.

Aidha, alisema isingekuwa busara kusitisha safari ya kwenda Samunge wakati tayari walikuwa wamefika Arusha, hivyo serikali imetumia busara kuwaruhusu.
Kwa upande mwingine alisema kuwa kuhusu usitishwaji huduma hiyo utawasumbua wengi, lakini itawapasa wasubiri hadi Jumatatu Mchungaji Mwasapila atakaporejesha huduma ya tiba.


Amina  Juma, Mkazi wa  Lindi, alisema aliwasili Arusha siku mbili zilizopita akisubiri kuruhusiwa kwenda Samunge na jana alifurahi kwa kuruhusiwa kwenda.
Alisema kwa upande wake anaona siyo busara kusitisha huduma hiyo hata kama ni kwa chache kwa sababu watu wanahitaji huduma siku na wagonjwa hawasubiri sikukuu ndipo waugue.

NIPASHE ilitembelea baadhi ya vituo vya magari ya kwenda Samunge jijiji Arusha na kushuhudia hali ikiwa shwari bila ya kuwepo msongamano wa magari na  abiria, hali iliyoashiria kuwa watu wamekubaliana na tangazo la Babu la kusubiri hadi wiki ijayo.
CHANZO: NIPASHE

No comments: