ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 14, 2011

Vimini vya wabunge wanawake vijana vyalalamikiwa

Israel Mgussi, Dodoma
IDADI kubwa ya wanawake vijana,wanavaa mavazi yanayopingana na  maadili ya Bunge, jambo linalowafanya baadhi yao kuzuiwa kuingia mara tu wanapofika katika milango mikuu ya kuingilia bungeni.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya wabunge wa kike vijana kulalamika kuwa wanazuiwa na walinzi kuingia bungeni, kwa sababu ya mavazi yanayopingana na  maadili ya Mtanzania na picha halisi ya Bunge.Hatua ya walinzi kuwazuia wabunge hao, iliwafanya waazimie kuwasilisha kilio chao kwa Naibu spika wakidhani kuwa wanaonewa.


Baadaye habari hizo zilimfikia Ndugai ambaye alizitolea maelezo kabla ya kuahirisha Bunge.Ndugai alisema, baadhi ya wabunge hasa wanawake, wamekuwa na tabia ya kuvaa mavazi yanayopingana na utamaduni na maadili mema ya Mtanzania.Kwa mujibu wa Naibu spika,baadhi ya mavazi hayo yanaonyesha  maungo ya miili ya wabunge hao na mengine ni mafupi mno.

"Kuna tatizo la mavazi, wabunge wengi wamekuwa wakisumbuliwa pale wanapofika getini wakitakiwa warudi wakabadilishe mavazi, sina tatizo la wabunge wa kiume, mavazi yao yanajulikana na hayajatupa taabu, hatuna tatizo na wabunge wanawake wakinamama hawa mavazi yao yamekuwa ya heshima," alisema Ndugai.

"Tatizo ni kwa wabunge wanawake vijana, hawa wengi wao wamekuwa wakivaa nguo fupi, zinazobana na zinazoonyesha maungo yao ya mwili, hii imekuwa ikitupa taabu sana,"alisema Ndugai.

Alisema kanuni za Bunge zimetaja mavazi yanayostahili kuvaliwa na mbunge anapouwa katika shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria."Niseme kuwa msione kama mnaonewa pale mtakaporudishwa pale getini,hizo ni kanuni na kwa kweli si vizuri kuvaa mavazi ambayo yatawafedhehesha wenzako na wewe mwenyewe pia,"alisema Ndugai.


CHANZO:MWANANCHI

No comments: