
Karibuni katika kilinge hiki cha mahaba kinachokwenda kwa jina la Mashamsham, najua kuwa wengi wenu mmekuwa na hamu kubwa ya kujua leo nimewaandalia nini.
Leo ninawaletea mada kama inavyosomeka hapo juu, Wanaume wanakuacha mara kwa mara? Ndiyo kuna wanawake wanapoingia kwenye uhusiano na baadhi ya wanaume hawadumu baada ya siku mbili tatu, wanajikuta wanapigwa kibuti na hawajui sababu hasa ni nini.
Leo ninawaletea mada kama inavyosomeka hapo juu, Wanaume wanakuacha mara kwa mara? Ndiyo kuna wanawake wanapoingia kwenye uhusiano na baadhi ya wanaume hawadumu baada ya siku mbili tatu, wanajikuta wanapigwa kibuti na hawajui sababu hasa ni nini.
Utakuta mwanaume ambaye alikuwa akikuita ‘sweetie’, ‘honey’ au ‘baby’ baada ya siku mbili anakukwepa na hataki kukusikia wala kukuona.
Kama yamekukuta, basi utakuwa na matatizo, inakubidi ujiangalie kwa jicho lako la tatu, inawezekana kabisa macho yako mawili yameshindwa kubaini udhaifu wako.
Unajua nini kinasababisha uachwe? Hebu fuatilia maelezo hapa chini:
Unapiga sana mizinga?
Inawezekana wewe unaendekeza sana fedha kwa kuiweka mbele kuliko kitu kingine chochote, mbaya zaidi huna mapenzi ya dhati na mara nyingi kwako fedha ina thamani kuliko mapenzi.
Kuna wanaume hawapendi kuombwa fedha mara kwa mara hata kama wanazo, wengi wanapenda kutoa kwa hiari yao pale wanaporidhika na kiwango cha tabia na uvumilivu wako na jinsi unavyowatumikia.
Hakuna ubishi kwamba kuna wanaume washenzi wa tabia katika mapenzi lakini kuna wanaume wengine wanaojua kulipa fadhila pale wanapofadhiliwa hasa haja zao.
Kama mtoto wa kike, haipendezi kuanza kunyoosha mkono mbele kuomba fedha kwa kuwa eti, umetoka ‘kuchakachua’ na mwenzi wako.
Au ‘unamlia taimingi’ baada ya siku mbili unampiga kirungu cha nguvu ili kufidia penzi, huo ni upuuzi. Ukiwa wa aina hiyo basi usilie siku watu wakiamua kukuruka viunzi.
Mapenzi hayathamanishwi na fedha hata siku moja, bali inatakiwa mwanaume akupende na wewe umpende kwa moyo mmoja siyo kwa kumfanyia vioja.
Unatoa sana matatizo?
Inawezekana una matatizo mengi ya kifamilia, mahitaji yako binafsi nk. Je, unapokutana na mwanaume siku za mwanzo na kuanza kumtolea shida za familia yako yote ni sahihi? Hakika si sawa.
Kama ndivyo, hata siku moja hutaweza kudumu katika uhusiano kama kila shida yako itafika kwa mwanaume ambaye penzi lenu ndiyo kwanza linachanua.
Hakuna mwanaume ambaye anaweza kukuvumilia, wengi wao hawapendi kubebeshwa mizigo ya familia yako mapema.
Ni vyema kusaidiana katika mapenzi lakini siyo kwa staili hiyo ambayo wanawake wengi wa mjini wanayoitumia.
Una manjonjo gani?
Hebu jiulize wewe unayesoma mada hii, ukiwa katika mashasham na mwenza wako unakuwa na majonjo ya namna gani?
Kuna wanawake wanapenda kujitia ufundi wasiokuwa nao, utakuta wanalia wakati machozi hayatoki, wengine wanajitia kupiga kelele huku mioyo yao inacheka!
Tafadhali kuwa kawaida, usijifanye unajua wakati hujui, dada’ngu wanaume wanapenda uhalisia wa mtu na siyo fujo zisizo na maana.
Wengi wao siku hizi wanajua tofauti ya makelele ya kweli na yale ya kuibiwa, hivyo jiadhari usilie pale usipolizwa na wala usipige kelele zisizo na msingi na usitoshe usiseme unaumia wakati wala mbu hajakuuma.
Unaweza kuona ni kitu kidogo, lakini kikamkera mwanaume wako na kuamua kukuacha kutokana na mbwembwe zako zisizo na maana.
Wiki ijayo itaendelea.
No comments:
Post a Comment