.jpg)
Zaidi ya abiria 38 waliokuwa wakielekea kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile maarufu kama babu, wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wanasafiri nalo kuacha njia na kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea juzi mchana hatua hache baada ya kuacha mto Selela wilayani Monduli, baada ya basi hilo aina ya Mitsubishi Fusso lenye nambari za usajili T276 BGH kutumbukia katika mtalo ulioko pembeni mwa barabara hiyo ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati
Hadi jana jioni abiria wote ambao wanatokea Muheza mkoani Tanga walikuwa wanasota katika eneo la ajali wakisubiri kupata usafiri mwingine kutoka Muheza kwani eneo hilo la ajali mpaka katika kijiji cha Selela ni zaidi ya kilometa tano
Nipashe imeshuhudia abiria wote wakiwa salama wakijipikia wenyewe chakula kutokana na kusafiri na magunia ya mkaa, chakula,mikeka pamoja na mahema
Jitihada za kumpata dereva wa basi hilo hazikuweza kufanikiwa kwani ilielezwa ameelekea Mjini Mto wa Mbu,umbali wa kilometa zaidi ya thelathini kwenye kituo cha polisi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment