Sunday, May 1, 2011

jumuhia ya watu waishio new york wapata viongozi

Mama Butiku akiombea mkutano upate baraka zake kutoka kwa Mwenze Enzi alie juu hii ilikua kabala ya uchaguzi kufanyika.
Jumuia ya Watanzania New york, New jersey na Connecticut wapata viongozi wake. kwa upande wa mwenyekiti nafasi imechukuliwa na Hajji Khamis baada wa kuwabwaga wapinzani wake kwa kula 37, na upande wa makamu mwenyekiti imechukuliwa na mwanamke pekee aliye jitokeza kugombea nafasi hiyo Dr Mariam Abu. na upande wa katibu nafasi imechukuliwa na Vincent Mughawai aliye pata kula 51, na nafasi ya umakamu imechukuliwa na Shaban Mseba, upande wa mtunza hazina imechukuliwa na kijana wa kizazi kipya aitwae Philip Lwiza kwa kubwaga mpinzani wake, na nafasi ya mtunza azina msahidizi imekwenda kwa mzee Temba. Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani mheshimiwa Ombeni Sefue....tuna wapongeza wale wote waliochaguliwa na tunanategemea maendeleo katika Jumuia hiyo. picha moja moja mpja viongozi hao wakila kiapo na picha ya pamoja ya viongozi wote baada ya kuapichwa mkutano huo ulifanyika nyumba kwa balozi uko Mt Vernon, New York, picha kwa hisani ya Ripota wa Vijimambo Ebra Nyagaly wa New York City..
Mwenyekiti Hajji Khamisi
Dr Mariam Abu makamu mwenyekiti
Shaban Mseba ambae ni naibu katibu,
Katibu Vincet Mughwai
mwenyekiti Hajji Khamis akishangilia ushindi wake....na wadau.
Kutoka kushoto ni Shaban Mseba ambae ni naibu katibu, Dr Mariam Abu ambae ni naibu mwenyekiti, Mwenyekiti ambae ni Hajji Khamis akiwa na mtoto wake akimpongeza baba yake kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuia hiyo, Anaefuatia ni balozi wa Tanzania nchin marekani Mh Ombeni Sefue,anaefana ni katibu Vincet Mughwai, mtunza hazina Philip Lwiza na msahidizi wake Mzee Temba

No comments: