ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 26, 2011

Mtoto azaliwa na vichwa viwili

MTOTO aliyekamilika viungo vya mwili lakini mwenye vichwa viwili amezaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu mkoani Shinyanga. 

Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Archie Hellah, alisema jana kuwa mtoto huyo mwenye jinsi ya kike alizaliwa juzi akiwa amekamilika viungo vyote ikiwa ni pamoja na miguu, mikono, shingo, lakini na vichwa viwili. 

Dk. Hellah alimtaja mama wa mtoto huyo kuwa ni Ngolo Magembe (22) mkazi wa Kijiji cha Ng’hoboko wilayani humo ambaye ujauzito wake ulitimia miezi tisa kama kawaida na ilikuwa mimba yake ya kwanza. 


‘’Kujifungua kwa mama huyo kulikuwa kwa matatizo kidogo, baada ya njia kuwa ndogo ililazimika kufanya jitihada za ziada ili kunusuru maisha yake na mwanawe kwa upasuaji lakini hata hivyo mtoto alikuwa ameshakufa, “ alisema Dk. Hellah. 

Tukio la kuzaliwa kwa mtoto mwenye vichwa viwili ni la kwanza kutokea kwenye hospitali hiyo tangu ianzishwe miaka kadhaa iliyopita. 

Dk. Hellah alisema mama wa mtoto huyo bado amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu na uchunguzi wa hali yake baada ya kujifungua kwa upasuaji.


CHANZO:HABARI LEO

No comments: