ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 27, 2011



Ndugu Wanajumuia,
Tunapenda kuwajulisheni kuwa ile safari iliyokuwa ifanyike tarehe 28 (siku ya Jumamosi mwezi huu) ya kwenda Mohegan Sun Casino, imeahirishwa mpaka siku ya Ijumaa June 17,2011.
New England Umoja inawaombeni samahani kwa usumbufu wowote ule utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya ambayo hatukuweza kuyaepuka.
Kwa wale watakaopenda kwenda tarehe 17 mwezi June, wawasiliane na Maria Sombe 413-364-8146 au Hamadi Mkambavange 413-221-2935. Pia kwa wale wenzetu wa maeneo ya Leominster/Fitchburg, tafadhali wasiliana na Saburi Eliamani 978-822-8192 au Siraji Mfangavo 978-413-1164.
Gharama za kila msafiri ni dola $30.00. Ada hiyo inakupatia "meal coupon"ya dola $10.00, ambayo inatosha kabisa kwa "buffet style dinner",na coupon ya dola $10 itakayokuwezesha kucheza tombola kwa wale watakaopenda kwenda kucheza tombola . Ukiangalia gharama halisi ni Dola $10 tu!!.
Siku ya Mwisho wa kupokea pesa ni June 10. Basi litaondoka saa kumi  na mbili jioni, na kurudi Saa 6 Usiku (12 AM).
Tafadhali kumbuka kuwa hii ni moja ya "Fund raising" ya kuadhimisha miaka 10 ya Jumuia yetu ifikapo July 3rd 2011. Ikiwa utakuwa umebanwa na hutaweza kujumuika nasi, basi tunaomba mchango wako wa dola $30.00 Tutafurahi sana ukipata nafasi ya kujumuika nasi kwenye safari hii. Tafadhali Usikose nafasi hii ya pekee na ya aina yake!!!.
YOU NEVER KNOW, IT COULD BE YOUR LUCKY DAY TO-BECOME A MILLIONAIRE!!!. Let's get ready to have some Fun!!!!!!
Karibuni sana wote

No comments: